Advertisements

Wednesday, October 18, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

               20 KIVUKONI FRONT,
                          P.O. BOX 9000,
                 11466 DAR ES SALAAM,  
                                   Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KUHUSU KUZINGATIA SHERIA KATIKA KUINGIZA AU KUTOA  MIFUGO NCHINI KWA AJILI YA MALISHO NA MAJI
Hivi karibuni, tumeshuhudia kuibuka kwa wimbi kubwa la uungizaji wa mifugo kutoka nchi jirani kuingia nchini kwa ajili ya malisho na maji bila kufuata sheria za nchi. Uingizaji wa mifugo kutoka nchi moja kwenda nyingine una madhara mengi, ikiwemo kiusalama, uharibifu wa mazingira na kueneza magonjwa ya mifugo.

Ikumbukwe kuwa tarehe 13 Oktoba, 2017, Wizara ya Mifugo na Uvuvi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitoa agizo la kuondoa mifugo yote iliyopo nchini kinyume cha sheria ndani ya siku saba (7). Kutofanya hivyo kutapelekea mifugo hiyo kutaifishwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kufuatia agizo hilo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatoa wito kwa Watanzania wote wenye mifugo nchi jirani wafuate taratibu za kisheria na kama kuna mifugo kwenye malisho nje ya Tanzania waiondoe mara moja ili kuepusha hasara na usumbufu.

Aidha, Wizara inatoa wito kwa Watanzania hususan wanaoishi Mikoa inayopakana na nchi jirani kuwa wazalendo kwa kutokushirikiana na raia wa nchi za kigeni kuvunja sheria mbalimbali za nchi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam

17 Oktoba, 2017

No comments: