ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, October 10, 2017

UTPC yawanoa waandishi wa habari Dodoma

Muwezeshaji wa mafunzo Deodatus Mfugale akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Centurion Nala Hotel Dodoma

Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo, Utafiti na Machapisho Victor Maleko akizungumza na waandishi katika Mafunzo hayo mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo hayo

Na.Vero Ignatus, Dodoma
Umoja  wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) inaeendesha mafunzo ya siku (5) yawaandishi  habari za mazingira (27)mkoani Dodoma, kwa waandishi kutoka mikoa yote nchini ikiwa ni awamu wa kwanza

Afisa program wa (UTPC) anayefanya kazi kitengo cha Mafunzo ,Utafiti na Machapisho Victor Maleko amesema kuwa  lengo kubwa la mafunzo hayo ni  kuwapata waandishi waliobobea katika kuandika habari za mazingira katika maeneo yao.

"Unapowapata wabobezi hawa ni rahisi kwa wadau wa habari kutoka mikoani kufanya kazi na waandishi amabao wapo madhubuti kwenye maeneo yao,wapo waandishi wengi makanjanja hawajui wanachokifanya"alisema Victor.

Mafunzo mengine yanayoendeshwa sambamba na haya ni pamoja na  mkoani Pwani yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Jinsia ,mkoani Morogoro yanaendelea mafunzo ya uandishi wa habari za Vijijini na mkoani Dodoma mafunzo ya uandishi wa habari za Mazingira

"tunataka tuwapate machampion watakao simamia habari za mazingira peke yayake,Jinsia  pamoja na  waandishi wa habari za vijijini tu"alisema

Amewaasa waandishi wa habari ambao hawajajiunga katika vilabu vya waandishi  habari vilivyopo kila mkoa wajiunge  kwani zinawasaidia kuwakutanisha pamoja watanufaika na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na UTPC ,ambapo amesema  mafunzo kama haya hayawezi kutolewa kwa mwandishi ambaye siyo mwanchama .

Kwa upande wake muwezeshaji wa mafunzo hayo Deodatus Mfugale amesema kuwa lazima mwandishi awe na malengo,waandike habari zinazoleta mabadiliko na zinazogusa hisia za jamii kwa ujumla.
''Mwandishi kama unaandika kila kitu muda wako unakaribia kwisha"alisema Mfugale.

Amesema kuwa UTPC itaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa habari chini ufadhili wa Ubalozi wa Sweeden hapa nchini kwa muda wa miaka (5) ambapo huu ni mwaka wa( 2) hadi 2020 wataendelea kubadilisha mafunzo hayo kadri ya  uhitaji wa waandishi .

No comments: