ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 26, 2017

WASHAURI WA MAHAKAMA WASEMA LULU ALIUA BILA YA KUKUSUDIA

Washauri watatu wa Mahakama Kuu wamesema msanii wa fani ya uigizaji filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu Lulu aliua bila ya kukusudia.
Washauri hao wametoa maoni yao leo Alhamisi Oktoba 26,2017 baada ya upande wa Jamhuri na wa utetezi kukamilisha kuwasilisha ushahidi.
Lulu ambaye yupo nje kwa dhamana anakabiliwa na kesi ya kumuua bila ya kukusudia msanii wa filamu, Steven Kanumba.
Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012 nyumbani kwa Kanumba, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.
Jaji Sam Rumanyika amesema hukumu itatolewa Novemba 13,2017.
Upande wa Jamhuri umewasilisha mashahidi wanne kuthibitisha shtaka hilo, huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi wawili, akiwemo Lulu.

Chanzo: Mwananchi

No comments: