Watu 7 wamefariki papo hapo na wengine 14 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongwa na lori la mizigo wakitoka kwenye sherehe ya harusi wilayani Hanang mkoani Manyara.
Ajali hiyo ambayo imetokea usiku wa Oktoba 14, 2017 imehusisha Noah yenye namba za usajili T 744 DJQ, likiwa limebeba watu wa familia moja, kugongwa na lori aina ya semi trailer lenye namba za usajili T449 CDR mali ya kampuni ya Lake Hill Paradise ya Singida, na kuleta majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu.
Licha ya watu walioshuhudia, manusura wa ajali hiyo ambaye ndiye bwana harusi aliyetoka kufunga ndoa, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bwana Wilson Simba ambaye pia amefariki, kutokuwa makini barabarani kabla ya kuchepuka upande mwengine.
Mganga wa zamu wa hospitali ya Tumaini Hanang, Bwana Chaokiwa Msangi, amesema wamepokea miili hiyo 7 na kuihifadhi chumba cha maiti, huku mmoja wa majeruhi ambaye ndiye bibi harusi akipewa rufaa ya kwenda hospitali ya Haydom, kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment