Advertisements

Thursday, October 19, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGUA MASHINDANO YA KUOGELEA YA KANDA YA TATU

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akiwasili katika shule ya Heaven of Peace kwa ajili ya kufungua mashindano ya kanda ya tatu ya kuogelea yaliyoshirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan pamoja na nchi za kanda ya nne ambazo ni  Afrika ya Kusini na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
 Waogeleaji kutoka Tanzania wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu yaliyofunguliwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe leo Jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa mashindano ya kuogelea kutoka nchi za Afrika Kusini, Sudan, Uganda, Zambia na Tanzania wakiimba wimbo wa taifa wa Tanzania pembeni ya bwawa la kuongelea wakati wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya kanda ya tatu ya kuogelea yaliyoshirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan pamoja na nchi za kanda ya nne ambazo ni South Afrika na Zambia leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Afrika Kusini na Zambia wakiruka ndani ya maji tayari kwa kushindana wakati wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu yaliyofunguliwa leo katika shule ya Heaven of Peace jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Afrika Kusini na Zambia wakionyesha umahiri wao wa kuogelea wakati wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu yaliyofunguliwa leo katika shule ya Heaven of Peace jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (watano kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa kuogelea pamoja na waratibu wa mashindano ya kuogelea ya kanda ya tatu baada ya kufungua mashindano hayo leo jijini Dar es Salaam katika shule ya Heaven of Peace na kushirikisha nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan pamoja na nchi za kanda ya nne ambazo ni  Afrika ya Kusini na Zambia leo jijini Dar es Salaam. Picha na Genofeva Matemu - WHUSM

No comments: