Advertisements

Monday, October 23, 2017

ZIARA YA MH. BALOZI WILSON MASILINGI JIJINI HOUSTON - TEXAS

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mh. Balozi Wilson Masilingi siku ya jana Jumapili ya tarehe 22/10 alifanya ziara ya kikazi katika jiji la Houston katika jimbo la Texas na kukutana na Watanzania wanaoishi jijini humo .

Katika ziara hiyo pia Mh. Balozi Masilingi alikutana na familia zilizoathirika na kimbunga cha Harvey ambacho kililikumba jiji Jimbo la Texas mwezi Agosti mwaka huu. Mh. Balozi Masilingi vilevile alikabidhi mchango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa familia hizo ambazo zilipoteza mali na wengine makazi wakati wa kimbunga.

Mkutano na Wanajumuiya wote ulifanyika katika Ukumbi wa Hotel Marriott uliopo Briarpark Dr. Houston, Texas . Pata picha za mkutano huo hapa chini.

Mh. Balozi WIlson Masilingi akiongea na wana-Houston
Mh. Balozi Masilingi akiwasalimia Watanzania wa Houston

Rai wa Jumuiya ya Watanzania wa Houston (THC) akimkaribisha Mh. Balozi Masilingi


Mh. Balozi Masilingi akiwa na Rais wa THC Bw. Mayocha



Viongozi wa THC wakiwa na Mh. Balozi Masilingi, kutoka kushoto ni
Bw. Lambert Tibaigana (THC Vice President), Mh. Balozi,
Bw. Mayocha (THC President) na Bw. Cassius Pambamaji ( THC Spokesperson)



















Bw. Kasapira akiendesha mitambo




Afisa Ubalozi Bw. Bw. Alfred Swere akijitambulisha kwa wana-Houston




Meza kuu


































































2 comments:

Anonymous said...

Kama kawaida Serikali yetu haiko makini... tokea mwezi wa nane ? Wananchi tuko makini na tunasaidiana pamoja na kuwasaidia viongozi wetu wanao tutetea wakipigwa na WATU WASIOJULIKANA.

Anonymous said...

Watanzania tusipende kulaumu Serikali kila kitu, kama Mtanzania ulienda kuishi ughaibuni kwa sababu zako binafsi, na ukatokea ukaugua kwa ugonjwa wa kansa, HIV, Homa, ugonjwa wowote au ukapatwa na matatizo ya kuuawa ni jukumu lako binafsi na familia yako na vyombo vya dola vya nchi na sehemu uliyoko kukabiliana na tatizo lililokupata, sio jukumu la Serikali ya Tanzania, kama ulienda Ughaibuni kwa kutumwa na Serikali ya Tanzania hapo ndipo Serikali inahusika, au kama ulienda ughaibuni ukaenda kujisajili kwenye Balozi ya Tanzania hapo ndipo Serikali itafatilia, tusipende kulaumu wakati hatufati taratibu zilizoko