Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amekiri kuwepo na vitendo ambavyo siyo sahihi ambavyo vilivyojitokeza katika Uchaguzi wa marudio katika baadhi ya kata na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe.
Nape amefafanua hayo baada ya kuwepo na malalamiko hayo kutoka upande wa upinzani ambapo amesema kwamba vitendo hivyo vinapaswa kushughulikiwa kisheria kama wahalifu na siyo kushughulikiwa kisiasa na kwamba kufanya matendo hayo kisiasa ni njia za kuficha uovu.
Pamoja na hayo Nape ameongeza kwamba hajawahi kuwa muumini wa matumizi ya nguvu kwenye siasa na wala hajawahi kushiriki mipango ya kutumia nguvu bali anaamini katika matumizi zaidi ya nguvu.
Aidha Nape ameongeza kwamba sehemu zote alizofanya kampeni na wala hakubariki matumizi ya nguvu hivyo kuwashauri vyama vya upinzani wafanye tathmini ya kweli kisha kuchukua hatua pale walipoteleza katika uchaguzi.
"Rafiki zangu Upinzani fanyeni tathmini ya kweli halafu chukueni hatua pale mlipoteleza. Hichi kinachoendelea cha kutoa visingizio vya jumla. Sikatai kuwa kulikuwa na baadhi ya maeneo kumekuwa na vitendo si vya kibinadamu lakini si kwa kata zote. Vitendo hivyo vishughulikiwe specific kisheria kama wahalifu na si kushughulikiwa kisiasa".Amesema Nape
No comments:
Post a Comment