Tume ya taifa ya uchaguzi imevitaka vyama vya siasa na wadau mbalimbali wa uchaguzi kuhakikisha uchaguzi mdogo wa madiwani unakaofanyika leo unafanyika kwa amani na utulivu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika kata zinazohusika na uchaguzi huo .
Akiongea jijini Arusha Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi jaji Semistocles Kaijage amesema wapiga kura wapatao 333,309 wanatarajiwa kupiga kura kuwachagua madiwani katika kata 43 za Tanzania bara na kuongeza kuwa uchaguzi huo utafanyika katika vituo 884.
Katika uchaguzi huo tume imeruhusu vitambulisho mbadala kwa wapiga kura waliopoteza au kufutika au kuchakaa kwa kitambulisho cha mpiga kura viwe ni leseni ya udereva, kitambulisho cha uraia kinachotolewa na mamlaka ya utambulisho nchini, pamoja na pasi ya kusafiria ilimradi majina yafanane na yaliyopo kwenye daftari la mpiga kura.
No comments:
Post a Comment