Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia Lisa Heywood akibadilishana mawazo na Emma Thomas na Faustina Mwapinga ambao wote ni Maafisa Uuguzi wakati wa kambi ya upasuaji wa moyo ya siku tano inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Katika kambi hiyo wagonjwa 23 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua kati ya hao watoto 13 na watu wazima 10.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto wa miezi sita ambaye mishipa yake ya moyo ilikuwa na tatizo la kupeleka damu kwa wingi kwenye mapafu wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea JKCI. Hadi sasa jumla ya watoto watano na watu wazima wawili wameshafanyiwa upasuaji.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) wakati wa kambi maalum ya upasuaji ya siku tano inayoendelea katika Taasisi hiyo. Hadi sasa jumla ya wagonjwa saba wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto watano na watu wazima wawili.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakiendelea na kazi ya kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).
Picha na JKCI
No comments:
Post a Comment