Na.Vero Ignatus, Arusha
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi(WCF )umeandaa mkutano wa siku mbili utakaoanza kesho Jijini Arusha katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC ,ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni Mafaofidia:Haki ya Mfanyakazi na chachu katika uchumi wa Viwanda mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Kassim Majaliwa
Akizungumza na waandishi wahabari Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini (WCF) Dr. Abdulssalaam Omary amesema kuwa lengo kuu la mkutano huo ni kutoa taarifa ya mwaka ya mfuko ,kutathimini maendeleo na changamoto zinazoukabili mfuko ,kupokea maoni ya kuboresha huduma za mfuko pia mada mbalimbali za uelimishaji zitatolewa na wataalamu mbalimbali wenye uzoefu kutoka baadhi ya nchi barani Afrika na kutoka Shirika la kazi Duniani (ILO).
Hadi sasa Mfuko umekusanya zaidi ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya matibabu kwa wanachama,hadi sasa taasisi 11,705 zimekwisha kujiunga na mfuko huo 2,105 bado hawajajiunga na mfuko huo wa fidia,ambapo Mkurugenzi Omary amesema kwa sasa wanajikita kutoa elimu kwa wafanyakazi waelewe kuhusiana na mfuko,wanatakiwa wafahamu kuwa kujiunga ni lazima ili hapo baadae sheria itachukua mkondo wake.
Kwa upande wake Meneja matekelezo (WCF) Victor Luvena amesema kuwa Sekta za Umma pamoja na sekta binafsi zote zinatakiwa kujiunga katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi,waajiri wanatakiwa watume mchango wa wafanyakazi wao katika mfuko huo ambao ulianzishwa rasmi julai mosi 2015.
Ameeleza katika mkutano huo pamoja na mambo mengine ,mgeni rasmi atatunuku tuzo kwa waajiri waliofanya vizuri katika utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi.
No comments:
Post a Comment