Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba ( katikati) akizungumzia mikakati ya Serikali kuufanya mji wa Dodoma kuwa Kijani wakati akipokea hundi ya shilingi milioni mia moja kutoka Kampuni ya The Net Work kupitia mchezo wa bahati nasibu wa Tatu Mzuka ili kusaidia katika kukabiliana na Changamoto zinazokabili mazingira hapa nchini mapema leo mjini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Kampuni ya Tatu Mzuka Bw. Sebastian Maganga.kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Injinia Joseph Malongo.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba akipokea hundi ya shilingi milioni mia moja kutoka Kampuni ya The Net Work kupitia mchezo wa bahati nasibu wa Tatu Mzuka mapema leo mjini Dodoma ikiwa ni mchango wa Kampuni hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kulinda mazingira. Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Kampuni ya Tatu Mzuka Bw. Sebastian Maganga.kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Injinia Joseph Malongo.
Mkuu wa Mawasiliano Kampuni ya Tatu Mzuka Bw. Sebastian Maganga (kushoto) akieleza mikakati ya Kampuni hiyo katika Kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni mia moja ili kusaidia Serikali kupambana na changamotozinazokabili mazingira mapema leo mjini Dodoma.Katikati Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba.
Meneja wa TEHAMA wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw. Kabora Mboya ( kulia) akitoa maelezo kuhusu mchango wa michezo ya Kubahatisha katika kujenga uchumi.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia Mkutano wa Waziri nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba wakati akipokea hundi ya shilingi milioni mia moja kutoka Kampuni ya Tatu Mzuka ili kusaidia katika kukabiliana na Changamoto zinazokabili mazingira hapa nchini mapema leo mjini Dodoma.
(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma)
Serikali imepokea hundi ya Shilingi milioni mia moja kutoka kampuni ya The Net Work inayochezesha mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka leo Mjini Dodoma kama hatua ya kuunga mkono juhudi za serikali katika Kuboresha Mazingira.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya fedha hizo, Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba amesema kuwa fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
" Kwa kuzingatia umuhimu wa Serikali kuhamia Dodoma, tumeamua kuwa fedha hizi zitatumika katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa Kijani kupitia mpango maalum ambao tulishauandaa kama Serikali na sasa tunashukuru wadau hawa kwa kutuunga mkono" Alifahamisha Makamba.
Akifafanua, Mhe. Makamba amesema serikali imejipanga kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika dhana ya mazingira hapa nchini, hasa kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi.
Aliongeza kuwa sasa ni wakati muafaka kwa wadau kujitokeza kushiriki kikamilifu katika Kulinda mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho.
Kwa upande wake Mkuu wa Mawasiliano wa kampuni hiyo Bw. Sebastian Maganga amesema kuwa Kampuni yake itaendelea kuunga mkono Serikali kwa kuhakikisha kuwa wanachangia katika shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo mazingira.
" Mpango wetu umeanza kwa kuchangia shilingi milioni 100 kwa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, mchango wetu unalenga kusaidia uboreshaji na ulinzi wa mazingira ambayo ni muhimu kwa maisha ya Watanzania wote" Alisisitiza Maganga
Akifafanua, Maganga amesema kuwa Kampuni yake imetenga milioni 150 katika kusaidia jamii katika sekta za Afya, Elimu na michezo.
Tatu Mzuka ni mchezo wa Kubahatisha ambao umechangia zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kama kodi hivyo kuchangia katika kukuza uchumi.
No comments:
Post a Comment