ANGALIA LIVE NEWS

Monday, November 20, 2017

WAZIRI UMMY AWATAKA WAGANGA WAKUU WA MIKOA KUANZISHA ZOEZI LA WAZI LA UCHUNGUZI WA SARATANI YA KIZAZI KWA WANAWAKE.

 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  leo jijini Dar es salaam .
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya vifaa vya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam.
 Waziri  wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akipokea moja ya nyenzo za  kufundishia juu ya uchunguzi wa saratani ya kizazi kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kuchunguza saratani ya kizazi leo jijini Dar es salaam katikati ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .
 Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  leo jijini Dar es salaam .
Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu  (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa  Wizara ya afya, Jpiego na USAID wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  leo jijini Dar es salaam wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran na aliyevaa nguo ya pundamilia ni Afisa Afya kutoka USAID Bi. Ananth Thambinygan .picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
WAZIRI Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amewaelekeza waganga wakuu wa mikoa yote nchini kuanzisha zoezi la wazi la uchunguzi wa saratani ya kizazi angalau mara moja katika mwezi ili kusaidia kutokomeza tatizo kwa wanawake hilo nchini.
Hayo amesema wakati wa kupokea vifaa vya kuchunguza saratani vyenye thamani ya shilingi milioni 98  ambavyo vimetolewa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya JHPIEGO kwa kushirikiana na USAID ili kusaidia kupambana na tatizo hilo nchini.
“Angalau ifikapo Desemba 2018 nataka  vituo vya Afya vya Serikali  524  viwe vinatoa huduma ya matibabu ya awali ya Saratani ya mlango wa kizazi na kufikia  wanawake milioni 3 watakaopata huduma hii ili kuokoa wanawake wa vijijini  kwani mpaka sasa hivi tunavyo vituo vya afya  265 vinavyotoa huduma hii ” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa uchunguzi na kutoa chanjo ya Saratani ya mlango wa kikazi  kwa wasichana kuanzia miaka 9 mpaka 14 ili kuweza kupunguza vifo vitokanavyo na tatizo hilo kwani katika kila wanawake 100 vifo vinavyotokana na ugonjwa huo ni 32.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa katika kuongeza jitihada za  kupambana na ugonjwa huo Serikali imeongeza vituo vya afya 100 kutoka 343  hadi kufikia 443 mwaka huu ili kutokomeza tatizo hilo nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Jhpiego nchini Tanzania Bw. Jeremia Zoungran amesema kuwa walianzisha mpango wa kupambana na tatizo hilo na kufanikiwa kuwafikia wanawake elfu 75 kwa mikoa 4 tangu mwaka 2009.
“Mbali na mikoa hiyo 4 bado tunalengo la kuongeza mikoa mingine 7 ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ajili ya kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kuokoa wanawake wengi zaidi nchini” alisema Bw. Zoungran.

No comments: