ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 28, 2017

ALIYEONGOZA KAMPENI KUMTOA MUGABE MADARAKANI ATEULIWA KUWA MAKAMU WA RAIS

Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Zimbabwe ambaye aliongoza kampeni za kumwondoa madarakani Rais wa zamani, Robert Mugabe ameapishwa kuwa Makamu wa Rais.
Ameapishwa Ikulu leo Alhamisi Desemba 28,2017 akiwa miongoni mwa makamu wawili wa Rais.
Jenerali Constantino Chiwenga (61), ameapa akiahidi kutii, kulinda na kutetea Katiba ya Zimbabwe.
Katika kiapo, Jenerali Chiwenga alisema, “Nitatekeleza majukumu yangu kwa nguvu zangu zote na kwa maarifa yangu yote na kwa uwezo wangu wote.”
Jenerali Chiwenga alistaafu jeshi wiki iliyopita ikiwa ni mwezi mmoja tangu vikosi vya jeshi kuchukua uongozi wa nchi kwa muda na kutoa shinikizo kwa Mugabe kuachia madaraka.
Kembo Mohadi, mwanasiasa wa siku nyingi ambaye pia amewahi kuwa waziri wa usalama wa Taifa naye ameapishwa kuwa makamu wa pili wa Rais.

No comments: