Madee alikuwa katika ziara ya kawaida ya kimuziki mkoani humo miaka kadhaa iliyopita, lakini akashangazwa na kipaji cha dogo huyu, ambaye kimsingi, alipaswa kuwa darasani shule ya msingi akisoma.
Alipomchukua na kumleta mjini na kumpa nafasi ya kuonyesha kipaji chake, kweli kijana wa Arachuga akaonyesha umahiri mkubwa na kila mmoja akamkubali. Ameingia kwenye game kirahisi sana katika umri wake mdogo.
Katika TipTop Connection, alikuwa ndiye msanii mdogo kuliko wote na kazi ambayo aliifanya, ilionyesha ubora wa hali ya juu kiasi cha kugeuka lulu. Kuna wakati, baadhi ya watu wakaanza maneno ya kumsema Madee kuwa alikuwa akimtumia dogo huyo kupiga hela.
Walikuwepo hadi watu waliomfuata dogo mwenyewe na kumweleza kuwa ananyonywa, kiasi kilichomfanya Dogo Janja atangaze kujitoa kwenye kundi hilo, tena huku akitoa maneno mabaya kwa Madee, akisema anafanya shoo nyingi lakini hapewi hela.
Watu wengi walikuwa upande wake alipotangaza kuondoka, wakiamini alipaswa kufaidika kwa kipaji chake. Ni kitu cha kawaida katika kazi yoyote, changamoto ni nyingi katika maisha, hivyo halikuwa jambo la ajabu baada ya kujifunza, akarejea tena TipTop na kuendelea na mzigo.
Juzikati Dogo Janja alishirikishwa katika tamthiliya iitwayo Sarafu, ambayo miongoni mwa vipande vyake, ni ile inayomuonyesha bwana mdogo huyo akifunga ndoa na Irene Uwoya, yule muigizaji mahiri wa filamu.
Awali, Dogo Janja alitaka dunia nzima iamini kuwa ni tukio la kweli, bila shaka akiamini itamsaidia kupata kiki katika harakati zake za kimuziki, lakini bahati mbaya, Uwoya, kwa kutambua kuwa ile ni sanaa na nje ya hapo yeye ana wazazi, ndugu na jamaa, aliweka wazi kuwa siyo ndoa halisi, bali ni maigizo.
Kitu cha kushangaza Dogo Janja ameendelea kung’ang’ania kuwa ile ilikuwa ni tukio la kweli, akijaribu hata kuwaingiza baadhi ya ndugu zake ili watetee.
Sijajua kwa nini bwana mdogo huyu anang’ang’ania
suala hili lililo wazi kuwa ni kweli. Kuna watu wanadai kimtindo, Dogo Janja anajipendelea kwa dada yetu huyu, huenda basi ndiyo maana anasema ni mkewe kwa maana hiyo.
Wakati mwingine inabidi nizungumze na Dogo Janja kama kaka yake mkubwa, ambaye ninafahamu madhara ya kutaka makubwa katika dunia iliyojaa mambo mengi.
Kuna suala la ushamba, ambalo nina uhakika linaweza kuwa linamhusu huyu bwana mdogo. Kwani hata kama ni kweli ni demu wako, kuna haja gani ya kupiga kelele kila siku za mke wangu mke wangu wakati ulimwengu mzima unajua hapo umeegesha tu?
Achana na umri, watu wanasema Dogo Janja ni mdogo kwa Uwoya, hii haiondoi ukweli kuwa katika mapenzi, kila jambo linawezekana, maana tunawajua wababa wengi tu wamefunga ndoa na vitoto vidogo, kama ambavyo vikongwe wengi pia ni wake wa vijana lukuki.
Ishu hapa unajipaisha kwa nani? Kuna wanawake wengine hapa mjini hupaswi hata kujitaja kuwa ndiye mwenye ‘mzigo’ maana unaweza kufedheheshwa bure. Unapiga kelele leo kuwa ni mkeo, kwa maana hiyo kesho tutakaposikia anatoka na mtu mwingine ndo tuseme umempa talaka au?
Wajanja huwa wanamega kisela, kimyakimya. Watu wenyewe hawa wa Bongo Movie siyo wa kuwawekea dhamana, leo wa kwako, kesho wa mwingine, Ney wa Mitego anawafahamu vizuri hawa viumbe au kama huelewi, basi muulize hata Idris Sultan.
Huenda anafanya utani labda, lakini hata kama ni hivyo anajichoresha!
GPL
No comments:
Post a Comment