ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 4, 2017

MBUNGE WA JIMBO LA MISUNGWI AMSHUKURU WAZIRI WA NISHATI

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaonyesha wananchi wa kijiji cha Mwaniko juu ya kifaa maalum cha uunganishaji umeme bila kutegemea mfumo wa waya (wireling system) kijulikanacho kwa jina la UMETA ikiwa na maana ya Umeme tayari, kifaa hiki kina uwezo wa kutoa huduma mbalimbalia kama vile kuwasha taa moja kwa ajili ya mwanga wa ndani , kuwasha Radio na Runinga ,inachaji simu, na kupasi nguo , kifaa hiki kinauzwa Tsh: 36,000 tu
Mbunge wa jimbo la Misungwi Charles Kitwanga akimshukuru Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kutokana na juhudi za kusambaza umeme katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya misungwi kupitia mradi wa REA awamu ya tatu (REA-III) , Mradi awamu ya kwanza1 & 2 jumla ya vijiji 224 vimepata huduma ya umeme na kufanya jumla ya idadi ya vijiji vyenye umeme kufikia 480 kati ya vijiji 758 vya mkoa wa Mwanza.

Kwa Mkoa wa Mwanza mradi wa REA awamu ya III unatarajia kusambaza umeme kwenye vijiji na vitongoji 278 na kuunganisha wateja wapatao 72,515.Kikao hicho kilifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

No comments: