Advertisements

Saturday, December 30, 2017

MHE MWANJELWA ATANGAZA KIAMA KWA WAFANYABIASHARA WANAOUZA MBEGU FEKI NCHINI

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Maabara ya Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Jana 30 Disemba 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro, Jana 30 Disemba 2017. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua Maabara ya Kutazama kiwango cha Uotaji wa Mbegu Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi alipotembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Jana 30 Disemba 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Mkoani Morogoro wakati wa ziara yake ya kikazi, Jana 30 Disemba 2017. 

Na Mathias Canal, Morogoro

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, Jana 30 Disemba 2017 ametangaza KIAMA kwa wafanyabiashara wa mbegu nchini wanaouza Mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali.

Amewataka wafanyabiashara wote wa mbegu ambao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa kuwauzia wakulima mbegu feki zilizopigwa marufuku na serikali kuacha haraka iwezekanavyo kwani serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo ya serikali.

Ametoa agizo hilo akiwa ziarani Mkoani Morogoro ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Taasisi iliyopewa jukumu na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la usajili wa wafanyabiashara wa mbegu (Seed Dealers).

"Serikali imepokea malalamiko mengi kwa wananchi kuhusu Ubovu wa mbegu jambo ambalo limepelekea kwa kiasi kikubwa kuwa na mavuno kidogo pasina kukidhi matakwa ya wakulima wetu nchini" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa

Naibu Waziri huyo pia ameiagiza Taasisi ya udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) kujitathmini kwa utendaji duni kwani wameshindwa kutimiza majukumu yao kwa kuwabaini wafanyabiashara wanaokiuka maagizo ya serikali pamoja na taratibu na sheria za nchi.

MWISHO
Aliwataka kuwafuatilia upya wafanyabiashara wote wa mbegu nchini ili kubaini wafanyabiashara wanaokiuka matakwa ya serikali na kutaka kukwamisha Juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameitaka Taasisi hiyo ya Udhibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI) kwa ushirikiano wa karibu na Wakala wa Mbegu nchini (ASA) kuhakikisha mbegu zinapatikana haraka ili kuwafikia wakulima tofauti na mfumo wa upatikanaji wa mbegu kwa muda mrefu.

Aidha, aliwaasa watumishi wote kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kuongeza Uadilifu, Uaminifu, Juhudi, Ubunifu, Nidhamu na Uzalendo katika utendaji kazi.

Alisema kuwa watumishi wote wa serikali wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano madhubutu kwa kufanya kazi spidi na viwango.

No comments: