Advertisements

Saturday, December 16, 2017

Taarifa kutoka Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Edmund Benard Mndolwa akitangaza kutengua ushindi wa Nuru Kassim Bainaga aliyetangazwa kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya  Wazazi kwenda kwenye Umoja wa Wanawake (UWT) na kumtangaza Zainabu Zubeir Sige kuwa mshindi halali wa nafasi hiyo Picha na Mpiga picha Wetu.

TAARIFA KUTOKA JUMUIA YA WAZAZI YA CCM
Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wake Ndg. Dkt. Edmund Mndolwa, leo tarehe 16 Desemba 2017 umekamilisha kuhakiki matokeo ya kura zilizopigwa katika Jumuia hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wajumbe wa Jumuia hiyo walioshiriki katika uchaguzi uliofanyika tarehe 13 Desemba 2017

Katika taarifa yake Ndg. Dkt. Mndolwa amesema matokeo yaliyotangazwa na kumpa ushindi Ndg. Nuru Kassian Bainaga kwa nafasi ya WAZAZI kwenda UWT, yanatenguliwa na badala yake, amemtangaza Ndg. Zainab Zuberi Sige kuwa mjumbe halali wa WAZAZI kwenda UWT.

Huu ni muendelezo wa kuhakikisha kuwa haki inatendekea katika chaguzi mbalimbali za Chama na Jumuia zake.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments: