WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI, BALOZI DKT. AUGUSTINE MAHIGA AKIMKABIDHI ZAWADI YA PICHA NAIBU WAZIRI WA BIASHARA WA CHINA MARA BAADA YA WAWILI HAO KUFANYA MAZUNGUMZO JIJINI BEIJING.
Na Mwandishi Maalum, Beijing
China imeahidi kushirikiana na Tanzania kikamilifu katika miradi ya kipaumbele ambayo Serikali ya AwamuyaTano imepanga kuitekeleza ili kufikia azma yake ya uchumi wa viwanda ifikapo 2020 na baadaye uchumi wa Kati ifikapo 2025.
Hayo yalibainishwa leo jijini Beijing na Naibu Waziri wa Biashara wa China, Mhe. Qian Keming na baadaye kukaririwa tena na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mipango (NDRC), Bw. Ning Jizhe walipofanya mazungumzo kwa nyakati tofauti na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
No comments:
Post a Comment