ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 21, 2017

USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOA WA MTWARA WASHIKA KASI

Wananchi mkoani Mtwara wamekuwa miongoni mwa wananchi katika mikoa 15 ya Tanzania ambao wanashiriki kwenye zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa lilionza mapema mwezi Novemba mwaka huu.

Kwa Wilaya ya Mtwara kwa sasa zoezi hilo linaendelea katika Kata za Magomeni na Ufukoni huku Kata za Shangani, Rahaleo, Tandika, Chikongola, Majengo, Reli na Vigaeni zikiwa zimekamilisha zoezi hilo. Wilaya nyingine ambazo zoezi hilo linaendelea ni Wilaya ya Masasi, Nanyumbu, Nachingwea na Newala.

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa mkoa wa Mtwara linategemewa kumalizika mwezi Februari 2018 kuruhusu kuanza kwa matumizi ya Vitambulisho hivyo huku nchi nzima zoezi hili likikusudiwa kumalizika mwezi Desemba 2018.

Mikoa mingine inayoendelea na zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa ni Iringa, Mbeya, Njombe, Songwe, Singida, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Kilimanjaro, Arusha na Lindi.
Mtendaji wa Mtaa wa Ufukoni – Mtwara akimthibitisha mmoja wa wakazi kwenye Mtaa wake kwa kumgongea mhuri wa Mtaa anakoishi kwenye fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa kabla mwananchi huyo hajaingia kwenye hatua ya mwisho ya kuchukuliwa alama za vidole, picha na saini ya Kielektroniki.
Baadhi ya wananchi katika Kata ya Magomeni mkoa wa Mtwara wakichambua fomu zao za Usajili kwa ajili ya kupigwa picha na kuchukuliwa alama za kibaiolojia.
Mkazi wa shule ya Msingi Lilungu mkoani Mtwara akipigwa picha wakati wa zoezi la kuwasajili wananchi kupata Vitambulisho vya Taifa likiendelea.
Mwananchi wa Kata ya Ufukoni akisubiri kupigwa picha wakati wa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa zoezi ambalo kwa sasa linaendekea katika shule ya Msingi ya Ufukoni mkoani Mtwara.

No comments: