ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 21, 2017

ZITTO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MBOWE

Katika kikao chake cha juzi, ambacho kiliamua kugomea ushiriki wa uchaguzi wa marudio, Kamati Kuu ya ACT Wazalendo iliuagiza Uongozi wa Taifa wa Chama kuwafikia wadau wote wa Demokrasia nchini na kuweka mikakati ya pamoja ya hatua za ziada za kuchukua ili kuboresha mazingira ya chaguzi za haki nchini kwetu, kwa kuanzisha mazungumzo na vyama vyote vya Upinzani nchini ili kuona njia bora zaidi ya mapambano ya pamoja ya kukabiliana na vitendo vya chama tawala cha kuvuruga chaguzi huru na za haki nchini.

Wakati Katibu Mkuu wa chama chetu, ndugu Dorothy Semu, anaendelea na utaratibu rasmi wa kulitekeleza hilo, nilipewa wajibu wa kuanzisha mazungumzo ya Viongozi wa Juu wa vyama hivyo. Jana, nimezungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, ndugu James Mbatia aliye hospitalini KCMC baada ya ajali (namuomba Mola ampe afya njema), pamoja na kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, ndugu Freeman Mbowe.

Nafurahi kwamba mazungumzo yetu yameanza vizuri.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama – ACT Wazalendo
Disemba 21, 2017
Dar es salaam.

No comments: