ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 1, 2017

WAZIRI WA NISHATI AKAGUA NGUZO ZA UMEME


Meneja Msaidizi katika kitengo cha Uchemshaji nguzo cha Qwihaya cha mkoani Iringa Bw.Fred Ngwega akimpatia maelezo waziri wa Nishati Dr.Medard Kaleman juu ya mtungi wa kuchemsha nguzo unavyofanya kazi ndani ya kiwanda hicho pembeni wanaomsikiliza ni wafanyakazi wa kiwanda hichopamoja waandishi wa habari.


Waziri wa Nishati Dr.Medard Kalemani akikagua nguzo za umeme katika kiwanda cha Qwihaya cha mkoani Iringa ,tarehe 29/11/2017 waziri alifanya ziara ya kukagua uzalishaji wa nguzo cha umeme mkoani Iringa katika kampuni ya Qwihaya na Sao Hill kwa lengo la kujionea jinsi wanavyoweza kuzalisha nguzo.

Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani aliagiza Shirika la usambazaji Umeme nchini (TANESCO) pamoja na wakandarasi wa Wakala wa Usambazaji Umeme vijijini (REA) kutumia nguzo zinazozalishwa na kampuni za hapa nchini kwa asilimia mia moja mpaka pale zitakapo waishia. Kalimani alisema baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi na baada ya kutembelea viwanda hivyo kalemani alifanya kikao na uongozi wa kampuni hizo na kuwaelezea dhumuni la ziara hiyo, kuwa serikali inataka kujiridhisha juu ya uwezo wenu wa uzalishaji kuanzia kiwango cha siku, mwezi mpaka mwaka ili kusudi wakandarasi wa REA na shirika la Tanesco wakianza kuagiza nguzo kutoka kwenu wapate nguzo katika idadi , ubora na muda watakao taka kwa lengo la kufanikisha mradi wa Usambazaji Umeme vijijini awamu ya tatu.

No comments: