Advertisements

Saturday, January 13, 2018

JANA IJUMAA UONGOZI PAMOJA NA WANACOMMUNITY WA NEW YORK WAKIWA NYUMBANI KWA SOFHIA KUMFARIJI

Uongozi wa Community ya Watanzania New York pamoja na wanacommunity waliungana kwa pamoja nyumbani kwa Sophi kumfariji kutokana na kifo cha mama yake mzazi kilichotokea gafla huko nyumbani Tanzania. Sofhi Yona Luangisa ni mwanajumuiya wa New York, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha kina mama na kina dada wa hapa New York Twiga Ladies. Uongozi wa NYCT unaiombea familia ya dada Sophia kuwa na nguvu na matumaini katika tukio hili ambalo halina ushujaaa. Vivyo hivyo Uongozi unamuombea kwa Mungu Marehemu Mama Yona apumzike kwa amani. Amina!

Sophia ameondoka leo saa tano asubuhi kuelekea nyumbani Tanzania, tumuombee pia kwenye safari yake aweze kufika salama.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen


GASTON MKAPA
MAKAMU MWENYEKITI NYTC,
KWA NIABA YA UONGOZI. Hapa ni Mr Shilla Afisa wa ubalozi New York City akiwa na mama mwenye nyumba wakew aliungana na watanzania wengini kutoa pole nyumbani kwa Sophia Pelham NY.

Kwa picha zaidi hapa chini.
No comments: