ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 10, 2018

JIJI LA DAR ES SALAAM LASHINDA TUZO YA KWANZA BARANI AFRIKA YA HUDUMA BORA YA USAFIRI ENDELEVU MWAKA 2018 JIJINI WASHINGTON, D.C., MAREKANI


Mheshimiwa Wilson M. Masilingi, Balozi wa Tanzania katika nchi za Marekani na Mexico, alipokea Tuzo ya Huduma Bora ya Usafiri Endelevu Mwaka 2018 (Sustainable Transport Award) kwa Jiji la Dar es Salaam kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 09 Januari, 2018. Balozi Wilson M. Masilingi ameambatana na Naibu Katibu Mkuu (E) kutoka OR - TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda, Mwenyekiti wa Bodi ya DART, Profesa David Mfinanga pamoja na Mtendaji Mkuu wa DART Mhandisi Ronald Lwakatare.
Sehemu ya Hotuba ya Mhe. Balozi Masilingi inasema:
"On behalf of my Government and people of the United Republic of Tanzania, I would like to take this opportunity to express my sincere gratitude to the Respected Jury members for selecting Dar es Salaam City and honouring us with this prestigious “Sustainable Transport” Award. I also thank the Institute of Transportation and Development Policy (ITDP) for inviting us to this historical event, Sustainable Transport Award Ceremony 2018, in Washington D.C. in this great Country the United States of America.

I bring to this "Sustainable Transport Award 2018" Ceremony warm greetings and best wishes for this New Year from His Excellency Dr. John Pombe Joseph Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania. The Government and people of the United Republic of Tanzania are greatly honoured to receive this prestigious Sustainable Transport Award 2018 given to the City of Dar es Salaam, Tanzania. We humbly and happily accept the Award as the first City in Africa to receive such an honour. Thanks to the Visionary and decisive leadership of our past President’s and the current President of our country H.E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli. The Exemplary take off of our six phased Dar es Salaam Bus Rapid Transit Project (DART System) is due to their good leadership. We also sincerely thank our partners the World Bank and the Institute for Transportation and Development Policy (ITDP) for the cooperation and support in raising the required finances and technical guidance to achieve sustainable transportation."
Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi akitoa hotuba ya shukurani, kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu (E) kutoka OR - TAMISEMI Bw. Tixon Nzunda

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akishika tuzo pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya DART, Profesa David Mfinanga na Mtendaji Mkuu wa DART Mhandisi Ronald Lwakatare.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiwa na viongozi wa ITDP (The Institute for Transportation and Development Policy) na washindi wa Tuzo wa miaka iliyopita.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi, Bw. Tixon Nzunda, Mhandisi Ronald Lwakatare, Profesa David Mfinanga pamoja na Watanzania walioshiriki waishio Marekani katika hafla ya kupokea tuzo.

Mhe. Balozi Wilson Masilingi akiwa katika katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa Taasisi ya kutoa Tuzo "Institute for Transport and Development Policy (ITDP)"

1 comment:

Anonymous said...

Mmmh magar ya kugombania hv. Hiyo Tuzo imepatikana vipi????