ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 25, 2018

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA AKUTANA NA WATENDAJI WA ASASI YA INTERNATIONAL YOUTH FELLOWSHIP JIJINI DAR

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akiteta jambo Ofsini kwake na Maafisa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship(IYF), leo Januari 23, 2018 walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza ambapo Watendaji wa Asasi hiyo wamewalisha mada kuhusu mafunzo yanayolenga mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo magerezani.
Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF), Jeon Hee yong akitoa mada mbele ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kuhusiana na mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu mara wamalizapo vifungo vyao magerezani
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mada kutoka kwa Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF) katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila..
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa taarifa fupi kabla ya Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship (IYF) kuwasilisha mada yao katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo Januari 23, 2018.
Kikundi cha Kwaya cha Asasi ya International Youth Fellowship ambacho kinaundwa raia kutoka nchini Korea kikitumbuiza kabla ya uwasilishaji wa mada kama inavyoonekana katika picha.
Wataalam wa Jeshi la Magereza wakifuatilia Mada kuhusu mabadiliko ya mitizamo kwa wafungwa katika kuachana na tabia za kihalifu.

Kamishna Jenaerali wa Magereza Nchini, Dkt. Juma Malewa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Asasi ya International Youth Fellowship walioketi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi Mkazi wa Asasi hiyo Bw. Jeon Hee yong(wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Tusekile Mwaisabila. Wengine waliosimama mstari wa nyuma ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza, leo Januari 23, 2018 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments: