ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 23, 2018

MASHINDANO YA BAISKELI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KUFANYIKA NCHINI TANZANIA

Mwenyekiti wa Michezo ya Jumuiya za majeshi ya Afrika ya Mashariki, Brigedia Jenerali Martin  Kemwanga amesema kuwa mashindano ya baiskeli yanajenga umoja kwa nchi za afrika Mashariki. 

Kemwanga ameyasema hayo alipokuwa anawakabidhi bendera ya nchi za Afrika Mashariki pamoja na kutangaza mshindano ya baiskeli yatayofanyika April 13 Mjini Zanzibar na Kumalizika wilayani Masasi mkoani Mtwara, amesema kuwa mashindano hayo kwa kauli mbiu ya Amani na Usafi wa Mazingira yanajenga umoja kati ya nchi wanachama. 

Amesema kuwa mashindano hayo yamekuja wakati wa mwafaka wa kutangaza fursa ya viwanda kwa nchi zitazoshiriki mashindano hayo pamoja na kutangaza umoja na  pamoja na  wananchi kuingia kwenye nchi hizo bila vikwazo vya aina yoyote. 

Rais wa Chama cha Mchezo wa Baiskeli Tanzania, Godfrey Mhagama amesema kuwa katika mashindano hayo nchi zitazoshiriki za Afrika Mashariki ni Tanzania ambaye ndie mwenyeji ,Kenya , Uganda , Rwanda , Burundi pamoja na Sudan Kusini na nchi wa Waalikwa ni Zambia na Ufaransa na nyingine zitajitokeza. 

Amesema kuwa wadau wa wajitokeze katika kufadhili mashindano hayo kwani muda bado wa kutosha ili waweze kufanikisha mashindano.
Mwenyekiti wa Michezo ya Jumuiya za majeshi ya Afrika ya Mashariki, Brigedia Jenerali Martin  Kemwanga  akizungumza na waaandishi wa habari mara baada ya kuwakabidhi viongozi bendera ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa ajili ya mashinano ya mchezo wa baiskeri yatakayofanyika nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Afrika Mashariki Fest, Kisembo Ronex Tendo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano ya baiskeri yatakayofanyika nchini Tanzania ili kuhamasisha Amani kwenye nchi za Afrika Mashariki.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Baiskeli Tanzania, Godfrey Jax Mhagama akizungumza na kuhusu ujio wa nchi mbalimbali za Afrika mashariki kwenye mashindano ya Baiskeri yatakayofanyika nchini Tanzania
Mwenyekiti wa Michezo ya Jumuiya za majeshi ya Afrika ya Mashariki, Brigedia Jenerali Martin  Kemwanga akimkabidhi bendera ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa Rais wa Afrika Mashariki Fest "Tanzania Chapter", Peter Nzunda wakati wa mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Afrika Mashariki Fest "Tanzania Chapter", Peter Nzunda akizungumza na waandishi wa habari jinsi walivyojipanga kwenye mashindano ya uendeshaji wa basikeri yatakayofanyika nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya AICC,  Balozi Dk.Ladislaus Komba akitoa amasa kwa waendesha baiskeri pamoja na uongozi huo ili waweze kufanikisha mashindano hayo vizuri.
Mkutano ukiendelea
Picha ya Pamoja 

No comments: