Hussein Makame-NEC
Katika
uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, mgombea udiwani kupitita CCM katika kata ya
Kimagai iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Mpwapwa mkoani Dodoma, amepita bila kupingwa.
Mbali
na uteuzi huo, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata sita za Tanzania
Bara wanatarajia kuteua wagombea wa udiwani wa kata hizo siku ya Jumatano ya
tarehe 24 Januari, 2018 kukamilisha kata 10 zilizopangwa kushiriki Uchaguzi
Mdogo wa Februari 17, 2018.
Akizungumzi
uteuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Hamis Mkunga amesema mgombea huyo wa CCM amepita bila kupingwa baada ya mgombea
wa CHADEMA kushindwa kurejesha fomu za uteuzi.
Amesema
katika uteuzi wa wagombea Jimbo la Kinondoni, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo
hilo amewateua wagombea 12 ambao ni ambao ni Godfrey Maliza kutoka chama cha TLP, Johnson Mwangosya (SAU) na Mwajuma Milambo kutoka UMD.
Mkunga
amewataja wagombea wengine walioteuliwa kuwa ni John January Mboya (Demokrasia Makini), Maulidi Mtulia (CCM), na Mary
Mpangala wa DP.
Wengine
ni Salim Mwalimu (CHADEMA), Rajabu Salum
(CUF), Mohamed Majaliwa (NRA), George Christian (CCK), Ally Omari Abdallah (ADA THADEA) na Ashiri
Kiwendu wa AFP
Kuhusu
uteuzi wa wagombea ubunge katika Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro, Mkunga amewataja
wagombea wanne walioteuliwa kuwa ni Dk Godwin Mollel (CCM) Mdoe Azania Yambazi (SAU),
Tumsifuheri Mwanry (CUF) naElvis Christopher MosiwaCHADEMA.
Katika
kata tatu zilizobaki, Mkunga amevitaja vyama vya siasa vilivyopitisha wagombea
ambao waliteuliwa katika kata ya Isamilo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Nyamagana mkoa wa Mwanza kuwa ni Chama cha CUF, DP, UDP, CCM, na CHADEMA.
Katika
kata ya Manzase iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,
wagombea walioteuliwa wametoka kwenye vyama vitatu vya CCM,CHADEMA na CHAUMA
wakati wagombea watatu waliteuliwa kutoka vyama vya ACT-Wazalendo, CCM na CUF
kugombea udiwani katika kata ya Madanga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Panganimkoa wa Tanga.
Kuhusu
pingamizi kwa wagombea, Mkunga amesema hadi saa 10:00 jioni ya Januari 21,
2018, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi walipokea mapingamizi
10 kutoka Jimbo la Kinondoni mapingamizi manne na Kata ya Isamilo mapingamizi
6.
“Hakuna
mapingamizi yaliyoripotiwa kutoka Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro na kata za Madanga
na Manzase” amesema Mkunga na kuongeza:
“Mapingamizi
ya Kinondoni, pingamizi moja limetolewa na CCM dhidi ya mgombea wa SAU, moja linatoka
chama cha Dp kwa mgombea wake, lingine limewekwa na mgombea wa CUF na wa CCM dhidi ya mgombea wa CHADEMA na la nne
limewekwa na mgombea wa CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM”
Amefafanua
kuwa katika kata ya Isamilo kulikuwa na mapingamizi sita mapingamizi manne ni
ya mgombea wa CCM aliyewawekea pingamizi wagombea wa CHADEMA, CUF, DP na
mgombea wa UDP.
Mapingamizi
mengine ni kutoka kwa mgombea CHADEMA dhidi ya mgombea wa CCM na pingamizi
lililowekwa na mgombea wa CUF dhidi ya mgombea wa CCM.
“Kinachofuata
kwa sasa ni hawa wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi
wanayapitia haya mapingamizi na kuyatolea maamuzi” ameeleza Mkunga na kufafanua
kuwa:
Amesema
kwa kuzingatia kifungu cha 44 (5) Sheria
ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292 na kifungu cha 40 (6) cha Sheria
ya Taifa ya Uchaguzi,wagombea waliokatiwa rufaa wana haki ya kukata rufaa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi.
Kata
sita zinazotarajia kufanya uteuzi tarehe 24 Januari, 2018 ni kata Buhangazaya Halmashauri
ya Wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera, na kata ya Kanyeleleiliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza.
Nyigine
ni kata ya Mitunduruni yaHalmashauri ya
Manispaa ya Singida mkoani Singida, kata za Kashashi, Gararagua na Donyomuruak
zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya
Siha mkoa wa Kilimanjaro.
Kutokana
na mgombea wa udiwani kata ya Kimagai kupitia CCM, kupita bila kupingwa, Mkunga
amesema Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani unaofanyika Februari 17, 2018
utahusisha majimbo ya Siha na Kinondoni na kata tisa badala ya kata 10 za
Tanzania Bara.
Katika
uchaguzi huo jumla ya vituo 869 vya kupigia kura vitatumika na wapiga kura 349,211
wanatarajia kushiriki katika uchaguzi huo mdogo.
Mkunga
amewaasa wagombea na vyama kuzingatie ratiba za kampeni kwa sababu kila chama
na mgombea wake kimewasilisha ratiba yake ya kampeni lakini pia tufanye kampeni
za kistaarabu kwani hilo ni suala la msingi sana.
Amevikumbusha
vyama na wagombea kuheshimu maadili ya uchaguzi katika kipindi hiki cha kampeni
kwani vyama vyote vimekubaliana kuheshimu maadili hayo na kuwaomba wananchi
wajitokeze kwa wingisiku ya kupiga tarehe 17 Febraur mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment