ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 12, 2018

MREMA AWAFIKISHA POLISI WALIOMZUSHIA KIFO

MWENYEKITI wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema amefika kituo cha polisi cha OysterBay kuripoti tukio la kuzushiwa kifo kupitia mitandao ya kijamii.

Mrema amedai waliozusha taarifa hizo walitaka wananchi wasisikilize mazungumzo aliyofanya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa badala yake wajadili kifo chake

“Lengo lao lilikuwa kuvuruga mkutano wa Lowassa na Rais ambao ulifanyika Ikulu, hivyo walikuwa hawataki watu wafuatilie ndiyo walijua wakisema Mrema amekufa watu wangekuwa bize na mimi kwa sababu mimi ni mashuhuri, na wasingehangaika na kile ambacho rais alichoongea na Lowassa” Mrema.

Pamoja na hayo Mrema amesema kwamba malalamiko yake mengine ni kwamba alipata usumbufu uliomfanya ashindwe kwenda mkoani Kilimanjaro ambapo alipanga kwenda kwa ajili ya kuwafanyia ibada wazazi wake waliokwisha tangulia mbele za haki ikiwa ni pamoja na kufanya misa ya shukrani kwa kupona ugonjwa uliokuwa ukimsumbua tangu kipindi cha uchaguzi.

Mrema amesema kwamba waliosambaza taarifa hiizo walisababisha mtafaruku kwa famiia na watu wengine ambao walianza kupata masikitiko kutokana na taarifa hizo ambazo zilianza kusambazwa siku ya Jumanne, Januari 9. Aidha amewataka polisi wachukue hatua kali kwa waliofanya hivyo na serikali isiwafumbie macho.

GPL

No comments: