Watatu toka kushoto ni Iddi Sandaly akiwa ameshikana mkono na Dullah baada ya kupatanishwa kwenye kikao kilichofanyika siku ya Jumaane Jan 2, 2018 Silver Spring, Maryland. Kikao kiliratibiwa na Ngalu (wa pili toka kushoto) wakiwemo wasuluhishi wengine Rebeca (kulia) ambaye ni mwenyekiti kamati ya kuratibu mkutano wa kuelekea uchaguzi DMV, Said Mwamende (hayupo pichani na Henry Kente (kushoto). Mkutano huo wa upatanishi ulifanyika kutokana na tuhuma zilizokua zikitolewa kwenye mitandao ya whatsApp na Dullah akimtuhumu Sandaly, Kikao cha jana kilikua cha kuwakutanisha wawili hao kuongea na kuyamaliza kama wanaDMV kitu ambacho kilifanyika na wawili hao kumaliza tofauti zao. Sifa nyingi kwanza ziwaendee Iddi na Dullah kwa kukubali kukaa chini na kuyamaliza na pili kwa Ngalu , Rebeca, Said Mwamende na Henry Kente kwa kufanikisha hili.

No comments:
Post a Comment