Advertisements

Tuesday, February 20, 2018

Dkt.Kigwangalla aitembelea familia ya Akwilina, Atoa ubani wa pole

Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo ametembelea nyumbani kwa familia ya Akwilina na kutoa ubani wa pole kwa msiba huo.

"Nimefika hapa kama Raia mwema tu ambaye nimeguswa na msiba huu na nimetafakari kwani na mimi kipindi fulani nilipitia chuo hasa kutoka familia zetu hizi masikini kwa hiyo inapotokea ukio kama ili unaona ni pigo kwa familia, pigo kwa jamii, pigo kwa wanafunzi wenzake na pigo kwa Taifa kwa ujumla wake" alieleza Dkt. Kigwangalla wakati akizungumza na vyombo vya Habari msibani hapo.

Dkt.Kigwanalla ambaye alifika msibani hapo majira ya saa saba mchana, aliweza kuungana pamoja na ndugu na jamaa wa wafiwa ambapo pia alipata chakula cha mchana pamoja na waombolezaji wengine sambamba na kutoa ubani wake kama mwananchi mwingine.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli ambaye yupo hapo kwa ajili ya kusimamia shughuli kwa upande wa Serikali, amebainisha kuwa wataendelea kuratibu baadhi ya mambo yanayoendelea hapo kwani msiba huo kwa namna moja Serikali imeguswa nao.

Mbali na Mkuu wa Wilaya hiyo, Wengine waliofika hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Ubungo, John Kayombo ambapo kwa pamoja na watendaji wengine wa Kiserikali wameweza kusaidiana na familia ya marehemu katika shughuli mbalimbali zinazoendelea msibani hapo.

Aidha, jana viongozi wengine waandamizi wa Serikali akiwemo Waziri Elimu, Mh. Ndalichako, Naibu Waziri wa Ulinzi Masauni na IGP Siro waliweza kutembelea kutoa pole katika familia hiyo.

Akwilina kabla ya kifo chake alikuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha siasa cha CHADEMA. 
Marehemu Akwilina enzi za uhai wake
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa pole kwa ndugu na jamaa wa familia ya Akwilina alipotembelea hapo kutoa pole
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akipata taarifa kutoka kwa ndugu Akwilina amabye alikuwa ni mlezi wa binti huyo.
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakiwa katika msiba huo
Waombolezaji wakipata chakula cha mchana msibani hapo
Viongozi wa Serikali wakipata chakula msibani hapo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya ndugu na jamaa walijitokeza katika msiba huo, Mbezi Luis, Jijini Dar e Salaam
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa tukio hilo
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makoli akizungumza na wanahabari wakati wa tukio hilo.

No comments: