Nilibahatika kusikiliza mahojiano ya Dr. Tlaa na Clouds ilinisikitisha hasa huyo balozi mtarajiwa kuongea mambo yasiyo ya kweli. Tukirejea nyuma nilimfahamu Padre Wilbroad Tlaa miaka ya mwanzoni mwa 1980 baada ya kuwa padre na kuhudumu parokia ya Sanu. Nataka nirejee historia ya Padre Wilbroad kwa sababu ambazo nitazitaja. Huyu padre kama mapadri wengine wanapitia mlolongo mrefu wa elimu kuanzia masomo ya sekondari ya kawaida huku Bible knowledge likiwa core subject" halafu Philosophy na Theology (elimu ya kumjua Mungu) alibahatika kwenda Urbaniana College ambapo alipata Shahada ya juu ya sheria za kanisa(J.C.D au Doctor inCanonic law) hii shahada ambayo alifanya kwa miaka mitatu baada ya kufanya diploma za Theology unaweza ukaita kama Doctor of Law ndiyo maana anaitwa Dokta Slaa. Wanasheria wa Marekani wengi wanazo hizo digrii lakini kwa upande wa sheria za kawaida mfano Barack Obama na Hillary Clinton wanazo hizo qualifications lakini kwa sheria za kawaida hivyo wangeweza pia kuitwa Dr. Obama au Dr. Clinton.
Mwaka 1984 kulikuwa na mapendekezo ya kuligawanya jimbo la Mbulu lililokuwa likiongozwa na mhashamu Askofu Nicodemus Hhando kuwa na jimbo lingine kwa upande wa Babati na kadiri ya mapendekezo walidhani Padre Wilbroad angekuwa Askofu wa jimbo hilo lingine, Bahati mbaya au nzuri jimbo halikugawanywa hivyo Wilbroad alibakia kuwa Vicar General wa jimbo la Mbulu akitegemewa kumrithi askofu Hhando, Haikuwa hivyo kukatokea hali ambayo sitaki kuongelea lakini baada Cardinal Pengo kumrithi marehemu Cardinal Rugambwa kulitokea tatizo ambalo hadi leo lipo pale Mbulu, warithi wa Hhando wamekuwa wakitoka nje ya Jimbo la Mbulu!
Mwaka 1985 kulitokea kulitokea msiba wa Herman Elias Sarwatt aliyekuwa spika wa bunge wa Africa Mashariki na mbunge wa kwanza wa Mbulu baada ya uhuru wa Tanganyika, msiba huo uliendeshwa na Padre Wilbroad Slaa ingawa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha wa wakati huo Charles Kilewo alimshukuru Padre Willy aliyeongoza mazishi kwa kumuita kama Padre John Nada (marehemu-Mungu amjalie mwanga wa milele), Padre Willy siku zote ni msemaji mzuri akamsahihisha mkuu wa mkoa akajisema yeye siyo John Nada. Mwaka huo aliandika kitabu kinachoitwa UTIMILIFU WA MWANAUMME nilibahatika kununua na kukisoma kwa makini, kilikuwa zaidi kama nadharia kuliko ukweli (The book was more hypothetical) sijui kama anakiamini hicho kitabu kwa yale aliyoyaandika mle hasa pale anaposema kuna urafiki wa kuchanjiana damu?
Niliifahamu familia ya Padre Willy(Hilo ndilo jina tulilokuwa tukimwita) kuanzia wazazi wake hasa baba mzee Qamara aliyekuwa akifanya kazi Gibbs Farm pale Karatu, wadogo zake Aloyce na Francis, mama alishatangulia mbele ya haki. Nilimwelewa Dr. Slaa kama padre mwenye msimamo na msomi lakini wakati jimbo lilivyoshindwa kugawanywa na yeye kubaki kwa muda kwenye nafasi ya vicar general na kuwa katibu wa baraza la maaskofu nilianza kuwa na wasiwasi kuwa pengine hawamtaki awe askofu labda kuna kitu sikijui kuhusu maisha yake ya binafsi, baadaye kukawa na surprise ya ghafla tukasikia ameacha upadre, tukasikia tena ameoa.
Bahati nzuri ninamfahamu Rose Kamili Sukums, ni jambo la faraja kuwa na familia lakini kuna ambao wameumbwa au tumeumbwa kutoridhika inaweza kuwa ni hulka ya binadamu hasa wale ambao tumezoea au wamezoea kuishi maisha ya kipekee pekee tunatafuta pale ambapo tutaona tumefika... kama ni maendeleo unakuwa na hamu ya kuendelea kuliko pale ulipotoka.
Padre Slaa akaacha upadre, akaenda ubunge(sitaki kuongelea historia yote) akaoa akaona bado hajaridhika na yale aliyotafuta......AKAOA TENA! Je ni haki kusema hana msimamo?
Maisha ya kisiasa ya Padre Willy yalikuwa na kupanda na kushuka kwingi (a lot of ups and down) Kutoka CCM kwa sababu za kuonewa yaani kunyimwa nafasi ya kugombea ingawa alishinda kura ya maoni dhidi ya Patrick Qorro hivyo kwenda CHADEMA ambapo alijipatia umaarufu mkubwa na baadaye kutuambia anaacha siasa (sina uhakika na hilo) na baadaye kurudi kufanya kazi serikalini kama balozi (anasema ameacha siasa) labda atabaki kama "independent ambassador" bado sijaelewa vizuri, Nitaelezea vizuri baadaye.
Msimamo wa Dr. Willy Peter Tlaa hautabiriki (Probably most unpredictable politician of all time), Anakuwa influence na mazingira, muda na waliomzunguka. Baada ya kuona hajapata nafasi ya kugombea urais akakasirika akaacha chama kwa sababu alichotegemea hakukipata hiyo ndiyo sababu kubwa, Akaacha upadre hakuridhika na mambo fulani fulani kama alivyowahi kusema, akaacha mke na watoto kwa sababu fulani fulani(sitaki kumuuliza Rose).
Msimamo wake unategemea anavutwaje na baadhi ya watu wake wa karibu ninamaanisha mke wake....Sababu kubwa ya kutokuwa na msimamo upande huo anaogopa kuachika, Ameshakuwa mzee kwa umri wa miaka 60 si rahisi kupata mke unayeweza kuishi naye mkaelewana hivyo hata kama mwenzi wako ni mkorofi inabidi Dr. Slaa awe mvumilivu! Je ni kweli anafuata upepo unapokwenda? Nitaeleza kwenye aya inayofuata.
Dr. Slaa alijiabisha mno wakati alivyolazimishwa aidha alivyopewa pesa au la....Naamini kuna "circumstancial evidence" alipewa pesa kuongea yale aliyoyaongea! Kwanza kutokana na utayarishaji wa maneno aliyoyaongea na uhusikaji wa Dr. Mwakyembe hadi Serena hotel walivyokuwa pamoja, pili kuondoka kwake kwenda Canada ilikuwa mipango ya serikali kama ambavyo tulivyoona kwa Lipumba alivyojiondoa UKAWA na kupelekwa Rwanda kwa muda ili maneno yaishe...watu wasahau, tatu pamoja na kusema alikuwa akipewa siri na usalama wa Taifa kitu ambacho technically ni uhaini kwake yeye na aliyetoa nchi nyingine huyo Slaa angekuwa jela leo hii! lakini serikali inajua amewafanyia kazi kubwa ya kumporomosha Lowassa hivyo wameachilia mbali, nne kitendo cha Dr. Slaa kumkashifu Frederick Sumaye waziwazi kwenye mkutano ule wa Serena hotel na kumwita mr. Zero YALE MANENO siyo ya Slaa, nina hakika kwa asilimia 100 aliambiwa aseme ili apunguze nguvu za UKAWA, kwa sababu kama Slaa alichukia Lowassa kuingia UKAWA mbona aliwa-target wengine wasiohusika kama Sumaye?
Kimsingi huwezi kumwita Sumaye Mr. Zero kama una akili timamu, Sumaye aliaminiwa na Mkapa na bunge na kukaa vipindi viwili (Hakuna waziri mkuu aliyekaa miaka kumi mfululizo zaidi ya Sumaye katika historia ya nchi yetu), Sumaye ana Diploma ya juu ya Egerton ya Agriculture Mechanization/Equipment ambayo ni sawa na degree na anayo Masters ya Leadership/ ya Chuo Kikuu cha kwanza duniani Harvard University huwezi ukamlinganisha na Dr. Slaa ambaye amesoma dini halafu anafanya siasa.....upeo wa Slaa upo kwenye dini tu halafu ana ubavu gani wa kumsema Sumaye?? Kujibu swali langu hapo juu, Slaa hana msimamo anafuata upepo unapoenda, ndiyo maana anavutwa kila mahali na wanawake( Kwa madai ya Mushumbusi kuwa Slaa alikuwa akionewa na mkewe wa kwanza) Naamini tena Slaa ni fuata upepo anavutwa huku anakwenda, huku anakuja n.k Hana msimamo. Kuna kipindi mkewe wa mwanzo alimfumania Dodoma akiwa na msichana muuza bar....Huyo siyo mtu mwenye msimamo.ANANUNULIKA!!!
Slaa "simply" yupo kwenye siasa wala si suala kudanganya watu, hiyo post anayopewa ni ya kisiasa hawezi kuwa "independent Ambassador" hata siku moja. Ninayo reference moja ninaye ndugu aliyeenda kuomba kwenye moja ya balozi zetu Tanzania swali la mwisho aliloulizwa ni kwamba je wewe ni mwenzetu hakuelewa maana yake.....akafafanuliwa je upo kwenye chama chetu?.....Sasa hapo utatenganishaje siasa na serikali? Balozi zetu zote zinafanya hivyo usipowapendelea chama tawala utaondolewa na sidhani Slaa ana huo ubavu.
Mwisho Dr. Slaa anapotosha umma kwa kusema eti KUPIGWA RISASI KWA TUNDU LISU NI JAMBO LA KAWAIDA NA KUPOTEA KWA WATU NI KAWAIDA. Huo ni uwongo...uwongo...uwongo mtupu ametolea mfano huko Canada alipokwenda. Slaa ni mpotoshaji wa kutupwa ndiyo maana nasema hana msimamo anabadilika badilika kama kinyonga.....Muulizeni angekuwa bado CHADEMA angesema ni jambo la kawaida kupigwa risasi kwa MWANASIASA?
Ni kweli watu wanapigwa risasi na kuuwawa au kujeruhiwa au kupotea kwa hasa Marekani na Ulaya ingawa kwa Canada siyo sana (Nitaelezea kwanini kwenye aya itakayofuata). Nchi zote nilizotaja watu wanapigwa risasi na kuuawa lakini SI KWA SABABU ZA KISIASA! Watu wanapotea lakini SI KWA SABABU ZA KISIASA , nchi hizi ni kawaida sana kumsema rais vibaya kwa kiasi chochote unachoweza, kuandamana mpaka Ikulu kwa nguvu zako na utalindwa na askari. Tanzania ukimsema rais kwenye mitandao utapotea au utapigwa risasi na kuuawa wapambe wa rais wakikasirika...bado tunakumbuka Azory Gwanda, Ben Saanane na Lisu.....HATUJASAHAU. Wanaopotea USA, Canada na Ulaya wanaibiwa kwa sababu tofauti na za kisiasa, period! Mauaji yanayotokea nchi hizi ni kwa ajili nyinginezo na wala siyo siasa, Angalau upelelezi unakuwepo na watu wanakamatwa na kuhukumiwa.
Tanzania hakuna upelelezi na hakuna wanaokamatwa ingawa wanafahamika, Je mbona Makonda alivamia Clouds alifanywa nini? Vipi kuhusu Jamaa yule aliyemtolea bastola Nape Nnauye mbona anafahamika yupo kwenye details ya Makonda, halafu Mwigulu anatuambia yule mara hafahamiki mara siyo askari....SASA KWANINI HAKAMATWI? Waliomkata Azzory Gwanda wanafahamika na gari walilotumia linafahamika linatumiwa na watu gani.....Hatupigi kelele tumekaa kama wanyama, tutaendelea kupotezwa kwa sababu watesi na wauaji wetu wanatujua vizuri....Sisi ni Waoga!
Dr. Slaa umewasiliti watanzania kwa unaloendelea kufanya. Ni aibu kujaribu ku-justify eti hata Canada watu wanauawa na kupotea, acha uwongo tuulize sisi tuliokaa huku miaka na miaka tunajua vizuri Canada kuliko wewe uliyeenda juzi, yote uliyoyasema ni uwongo....eti mawaziri wanafanya kazi tatu zingine kwenye stores?? Ni waziri gani wa Canada anayefanya kazi tatu unayemfahamu? Ndiyo maana nasema huna msimamo unafuata upepo una-justify kitu ambacho hakina ukweli.
No comments:
Post a Comment