TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania yaridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani
40 kwa wasafirishaji wa mizigo
Tanzania
imeridhia kufuta tozo ya Dola za Kimarekani 40 (USD40) inayotozwa kwa kila stika kwenye magari yanayosafirisha
mizigo kwenda nje ya nchi. Hatua hii imefikiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa
Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la
Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha
Akizungumza katika Mkutano
huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema
Tanzania imefikia hatua hii ikiwa ni moja ya jitihada za kuendelea kuboresha
mazingira ya biashara nchini na Jumuiya kwa ujumla.
Tozo
hii imekuwa ikitozwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa malori yanoyosafirisha
mizigo kwenda sehemu mbalimbali nje ya mipaka ya nchi. Baada ya tathimini Serikali
imebaini kuwa tozo hii inasababisha usumbufu na kuongeza gharama kwa wasafirishaji
wa mizigo. Hata hivyo hatua hii inaendelea kuifanya Tanzania kuwa mtekelezaji
mzuri wa makubaliano na itifaki mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano
huu uliofanyika kwa kipindi cha siku tatu tarehe 7 hadi 9 Februari 2018, pamoja
na mambo mengine ulilenga kujadili na kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya
kiushuru (NTBs) ambavyo vimekuwepo
kwa muda mrefu katika Jumuiya. Mkutano huu umefikia tamati leo katika Makao
Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Jijini Arusha.
Taratibu za kuanza kufuta
tozo hii zinaanza kutekelezwa mara moja.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
9 Februari 2018
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. CharleS Mwijage(Mb) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Dharura wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mkutano ukiwa unaendelea
No comments:
Post a Comment