ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 7, 2018

JESHI LA ZIMAMOTO MKOANI ARUSHA LAMUUNGA MKONO JPM




Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akipokea fire extinguisher toka kwa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kennedy Komba kwaajili ya nyumba za Polisi zilizojengwa mkoani humo.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Arusha limemkabidhi vifaa vya kuzimia moto (fire extenguisher’s) sita mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya nyumba za polisi zilizojengwa mkoani humo.
Akikabidhi vifaa hivyo kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamanda, Kennedy Komba amesema Jeshi hilo lina wajibu wa kuhakikisha ujenzi wa nyumba za makazi unazingatia vigezo vyote vya usalama, wao kama Jeshi wanaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuhakakikisha makazi ya askari polisi yanakua bora.
“Sisi kama Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Arusha tunaunga mkono jitihada za Amiri Jeshi Rais Magufuli sambamba na wadau wengine waliochangia ujenzi katika kuhakikisha nyumba hizi mpya za askari ambazo ziliungua moto miezi michache iliyopita zinakua salama kwa kuweka vizima moto katika kila nyumba kama matakwa ya usalama yanavyohitaji” alisema Kamanda Komba.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alipongeza sana jeshi hilo kwa kuonyesha moyo wa kujali jitihada za Rais Magufuli na wao kufanya kitu ambacho kinatuma ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia usalama dhidi ya Majanga ya Moto.


“Kwakweli nimefurahi sana kupokea hizi fire extinguishers kwaajili ya nyumba zetu za polisi pia tunafurahi kuona hata taasisi za serikali zikishirikiana na Mhe Rais kufanikisha mradi huu,pia uwekaji wa vifaa hivi unatukumbusha hata sisi tunapojenga nyumba zetu ni muhimu sana kukumbuka kuweka vifaa vya tahadhari kwani kinga ni bora kuliko tiba” alinukuliwa Gambo.

Ujenzi wa nyumba hizo 31 kwaajili ya makazi ya askari polisi umetokana na janga la moto lililosababisha jumla ya kaya 13 za askari katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Arusha kupoteza makazi na mali miezi michache iliyopita.
Mradi huu wa nyumba za polisi umegharimu zaidi ya shilingi milioni 540 ambapo shilijngi milioni 260 zimetolewa na Rais Magufuli.

No comments: