Mchungaji wa Mji Mtakatifu na kazi nyingine za Palestina na Jordan Theophilus III, kwa niaba ya wachungaji na viongozi wote wa Makanisa ya Jerusalemu (Makanisa ya Kigiriki, Kikatoliki na Kiarmenia), katika hatua ambayo haijawahi kutokea, Jumapili iliyopita ametangaza kulifunga Kanisa hilo la Ufufuo lililopo Jerusalemu ya kale hadi itakapotolewa taarifa nyingine, ikiwa ni kutokukubaliana na kupinga kwao na sera za utawala wa kivamizi wa Israeli dhidi ya Makanisa na kuyataka yalipe kodi.
Hayo yamesemwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika kiwanja cha Kanisa hilo la Ufufuo,ikiwa ni kupinga vitendo vya utawala wa kivamizi dhidi ya makanisa hayo. Kwani utawala huo hivi karibuni umeyataka Makanisa hayo ya Jerusalemu yalipe kodi ya mali ijulikanayo kama"Arnona",yenye thamani ya shekel milioni kila mwaka, huku ukiingilia mali za Kanisa la Orthodox la Kirumi kwa lengo hilohilo.
Nao Viongozi wa Makanisa ya Jerusalemu katika mkutano wa waandishi wa habari, wametoa tamko wakisisitiza ya kwamba,”Kuyatoza kodi Makanisa mjini Jerusalemu ni ukiukwaji wa mikataba yote iliyopo na wajibu wa kimataifa unaodhamini haki za Makanisa na mambo yake maalumu."
Tamko hilo limesisitiza kuwa, hatua hiyo ni "jaribio la kudhoofisha uwepo wa Kikristo katika jiji hilo," Huku likionya kuupitisha mpango wa kamati ya wizara iliyo chini ya utawala wa kivamizi wa Israeli wa kutoza kodi kwa Makanisa mjini Jerusalemu,ambao unafanyika kupitia kuchukua kwa nguvu ardhi ya Makanisa hayo yaliyo mjini hapo.
Serikali ya Palestina imeizingatia hatua ya utawala wa kivamizi kutoza kodi nyumba za ibada yakiwemo makanisa, kuwa ni uadui mpya dhidi ya wananchi na maeneo yake matakatifu, jambo lililopelekea kufungwa kwa kanisa la Ufufuo lililopo katika mji mkuu unaokaliwa kimabavu. Huku ukiuchukulia uadui huo mpya kuwa unalenga mji wa Jerusalemu na taifa letu lote la kiarabu la kipalestina pia unagusa maeneo yake matakatifu, huku likionya juu ya madhara makubwa yanayoweza kunyakua ardhi za makanisa.
Serikali imeomba kuingilia kati kwa haraka kwa jumuiya ya kimataifa ili kusitisha vitendo hivyo vya Israeli, ambavyo vinahesabiwa kuwa ni mashambulizi mabaya ya mikataba,makubaliano na desturi zote za kimataifa, vinavyodhamini uwepo wa uhuru wa kuabudu na kuheshimu utakatifu wa sehemu za kidini,katika hali yoyote na popote.
Serikali pia imetoa wito maalumu kwa ulimwengu wa kikristo na kiislamu, wa kuchukua hatua stahiki kwa ngazi zote ili kuzuia vitendo vya kivamizi, vinavyolenga kwa kiwango sawa sehemu takatifu za kikristo na kiislamu.
Kwa upande mwingine, mwanachama wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina Mheshimiwa ”Hanan Ashrawi” katika tamko lake rasmi alilolitoa, amelaani mashambulizi mabaya ya Israeli dhidi ya makanisa na sehemu takatifu za kikristo mjini Jerusalemu, ukiwemo uamuzi wa hivi karibuni wa Manispaa ya kivamizi kutaka kodi ijulikanayo kama"Arnona" kutoka katika mali za Kanisa lililopo Mji Mkuu unaokaliwa kimabavu.
Ashrawi amesema kuwa, “Makanisa ya Kikristo yapo katika ardhi hii muda mrefu kabla ya kuanzishwa kwa Israeli na kwamba utambulisho wa Palestina unajumuisha urithi wa kale zaidi wa Kikristo unaoendelea kuwepo, ukiwa ni sehemu ya uwepo wa Palestina wa asili katika ardhi hii. Dola ya Israeli kwa hatua hizi za hatari, inakiuka vibaya hali iliyopo ambayo ndio msingi wa hali ya makanisa ya kikristo nchini Palestinakwa karne nyingi”.
Ashrawi ameongeza kusema kuwa, sheria za Israeli za hivi karibuni zinakuja katika mazingira ya kuimarisha mwelekeo wa dola ya kivamizi, wenye sera za uhamisho wa nguvu na usafisho wa kikabila kwa lengo la kufuta uwepo wa Palestina na kuitenga Jerusalemu na eneo lake. Pia kwa makusudi na njia ya moja kwa moja huenezwa makanisa, akaunti na mali zake, ili kuimarisha udhibiti wa Israeli wa Mji Mtakatifu na kuongeza nguvu uwepo wa wayahudi wenye itikadi kali, kwa kuwaondosha wakazi wa asili wa mji huo.
Ameongeza kusema kuwa,hakika Israeli inafanya hasa uhamisho na kushambulia kwingine, kama ulivyo uvamizi wake wa kijeshi usio wa kisheria unakiuka moja kwa moja uhuru wa kuabudu kwa dini zote. Huku ikifanya ubaguzi mbaya kupitia sera zake zilizo rasmi dhidi ya wapalestina wakristo na waislamu kwa namna iliyo sawa.
Akasisitiza ya kwamba sera za Israeli, hatua zake na sheria zake,inaaibisha madai yake kuwa inalinda uhuru wa kuabudu kwa dini zote, tokea uvamizi wake Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza mwaka 1967, Israeli imewazuia kwa namna iliyoratibiwa wananchi wa Palestina wakiwemo wakristo na waislamu kufika katika maeneo matakatifu ya ibada yaliyopo mjini Jerusalemu, kama walivyowazuia wakazi wa Jerusalemu kupata huduma muhimu zikiwemo afya na elimu.
Katika mtiririko huohuo, Mamlaka ya Hashimiya ya Jordan imelaani hatua hiyo ya Utawala wa Kivamizi wa Israeli dhidi ya Makanisa ya Jerusalemu na mali zake, kiuzingatia Utawala huo kuwa unakiuka sheria za kimataifa,huku ikiutaka "Kuachana na hatua yake hiyo mara moja".
Hayo ameyasema Waziri wa nchi katika Mambo ya habari ambae pia ni Msemaji Mkuu wa serikali Mheshimiwa Muhammad Al Muumaniy,ambapo amesisitiza kutokukubaliana kabisa kwa Mamlaka hiyo na hatua hiyo ya Israeli iliyoratibiwa, katika kubadilisha hali ya kihistoria na kisheria iliyopo katika maeneo matakatifu mjini Jerusalemu ya Mashariki, zikiwemo mali na wakfu za kiislamu na kikristo.
Al Muumaniy amesisitiza kwamba,"Hakika hatua hizi zinapuuza sheria za kimataifa, sheria za kibinadamu za kimataifa na mpango wa hali ya kihistoria uliopo tokea miaka mingi",huku akiashiria kwamba "makanisa siku zote yamesamehewa kulipa kodi kwa tawala za kiraia zilizopo mjini". Ameitaka Israeli "kuacha haraka maazimio yake iliyoyapitisha dhidi ya Makanisa na kuheshimu wajibu wake kwa mujibu wa sheria za kimataifa,kama ndio nguvu inayoweka uvamizi katika Jerusalemu ya Mashariki.
No comments:
Post a Comment