ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 28, 2018

:Makamu wa Rais amsaidia mkazi wa Salasala Kiti cha Magurudumu

Msaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Nehemia Mandia (kulia)akizungumza na Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Machimbo ya Zamani Salasala kabla ya kumkabidhi Kiti cha Magurudumu kilichotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Bi. Sidonia Ntibashigwa mkazi wa Livingstone , Machimbo ya Zamani akikabidhiwa kiti cha magurudumu alichosaidiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Bi. Sidonia Ntibashigwa ambaye pia anafahamika kama Mama Sophia mkazi wa Machimbo ya Zamani, Sala Sala Mbuyuni amemshukuru Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia kiti cha magurudumu (wheel chair).

Mama Sophia ambaye alipata ya ajali ya kugongwa na roli tarehe 28 Mei, 2016 Mbuyuni, Salasala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi kiti hicho Msaidizi wa Makamu wa Rais Siasa Ndugu Nehemia Mandia alisema “Mheshimiwa Makamu wa Rais aliguswa na suala lako ambalo liliandikwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusiana na ajali uliyoipata na ulemavu ambao umekupata kutokana na ajali kutokana na kitendo hicho ameona akusaidie kiti cha magurudumu kwa ajili ya wewe kufanya shughuli ndogo ndogo unazoweza kufanya”.

Kwa upande wake Mama Sophia alishukuru sana kwa msaada huo wa Kiti na kumuomba Makamu wa Rais aendelee na moyo huo huo wa kusaidia wananchi wake .

Alisema kwa sasa bado anaendelea na matibabu kwa sababu mguu wake mmoja bado haujawa na nguvu hivyo hawezi kusimama.

Mama huyo mwenye watoto sita na wajukuu wanne alisema pia bado anahitaji msaada ili aweze kupata matibabu zaidi.

No comments: