MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikabidhi sim tanki ya lita 500 kwa viongozi
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu na afya jimboni humo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa bati na rangi kwa baadhi ya viongozi waliojitokeza kuja kuchukua masaada huo
MBUNGE wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimkabidhi diwandi makopo ya rangi
Na Fredy
Mgunda,Mufindi.
MBUNGE wa Jimbo la
Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi
vyenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni 12 vitakavyotumika kuboresha miundombinu
ya sekta ya elimu na afya jimboni humo.
Akizungumza wakati
wa ugawaji wa vifaa hivyo Mgimwa alisema kuwa ametoa mabati 280, mifuko 310 ya
saruji, rangi za maji na mafuta na sim tenki la lita mia tano (500) za
kuhifadhia maji.
“Nilifanya ziara
katika vijiji vya kata hizo nikaona wananchi wanavyojitoa kuboresha sekta
ya elimu na mimi kama mbunge wao nikaamua kuwaunga mkono kwa kuchangia vifaa
hivyo” alisema Mgimwa
Mgimwa alizitaja kata
zinazonufaika na msaada huo ni kata ya Mapanda, Kibengu, Ihanu na Sadani na akavitaja
vijiji vinavyonufaika na msaada huo kuwa ni pamoja na Ihimbo, Ukami na Chogo
katika kata ya Mapanda; na Kipanga, Igeleke, Kibengu, Usokami na Igomtwa katika
kata ya Kibengu.
Vingine ni kijiji
cha Lulanda katika kata ya Ihanu na katika kata ya Sadani Mgimwa sehemu ya
msaada huo inakwenda kusaidia ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya
sekondari Mgalo.
Aidha Mgimwa alisema kuwa ataendelea kusaidia maendeleo kwenye vijiji ambavyo
vinafanya maendeleo katika jimbo lake
Akiongea kwa
niamba ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi na vijiji vyote vilivyonufaika na
msaada huo, Makamu Mwenyekiti Asheri Mtono alisema kuwa jimbo la
Mufindi Kaskazini linakabiliwa na changamoto nyingi za ujenzi wa majengo
mbalimbali hivyo msaada alitoa utapunguza changamoto zilizopo kwa kiasi Fulani
“halmashauri hii
ina changamoto kubwa ya uchakavu wa miundombinu ya shule na kwa msaada huu wa
mbunge mazingira hayo yatakwenda kuboreshwa” alisema Mtono
Mtono ambaye pia
ni diwani wa kata ya sadani alisema pamoja na mchango wa mbunge huo na wadau
wao wengine, wananchi wa vijiji hivyo na vingine vyote katika halmashauri hiyo
wanahitajika kuendelea kuchangia shughuli zao za maendeleo.
Nao baadhi ya viongozi wa vijiji wamempongeza mbunge Mgimwa kuwa kutoa vifaa vya ujenzi
kwenye vijiji vyake vyote vya jimbo la Mufindi Kaskazini ambavyo vitachochoe
kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.
Mmoja wa wanufaika
wa msaada huo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Isupilo, Onorata Mwanuke alisema
kwa msaada waliopatapata wanakwenda kukamilisha ujenzi wa nyumba moja ya
mwalimu.
“Mahitaji ya
nyumba za walimu ni tisa zilizopo ni tatu na mbunge ametoa msaada wa mifuko 30
ya saruji kusaidia kukamilisha nyumba ya nne ya mwalimu. Tunategemea mbunge
ataendelea kutuunga mkono”alisema Mwanuke
Kabla ya jana
mbunge mgimwa alishakuwa ametoa jumla ya bati mia tano tisini (590) na
saruji mifuko mia mbili ishirini (220) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati
wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na walimu wa
shule zilizopo katika kata ya Ihalimba huku lengo likiwa kuboresha sekta ya elimu
na afya kwa wananchi.
Na alifanya kazi kwa
kushirikiana na wananchi wa kijiji cha Kibengu wametumia jumla ya
shilingi milioni mia moja kumi na tisa na laki mbili (119,200,000) katika
ujenzi wa madarasa ya shule,zahanati na nyumba za wafanyakazi wa zahanati na
walimu wa shule zilizopo katika kijiji hicho lengo likiwa katika kuboresha
sekta ya elimu na afya kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment