Mkuu wa Takwimu za Bei Zanzibar Khamis Abdul-rahman Msham akitoa maelezo kuhusiana na Takwimu za Bei ambapo zimeonekana kushuka kutoka asilimia 5.9 kwa Mwezi wa Disemba 2017 hadi asilimia 5.2 kwa mwezi wa January 2018 hafla iliofanyika Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Mjini Unguja.
Meneja wa Uchumi wa Benki ya Tanzania Tawi la Zanzibar Moto Ng'winganele Lugobi katikati akitoa ufafanuzi wa Baadhi ya maswala yaliouliza na katika hafla ya kutoa Takwimu za Bei ambapo zimeonekana kushuka kutoka asilimia 5.9 kwa Mwezi wa Disemba 2017 hadi asilimia 5.2 kwa mwezi wa January 2018 hafla iliofanyika Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Mjini Unguja.kulia yake ni Mkuu wa Takwimu za Bei Zanzibar Khmis Abdul-rahman Msham na kushoto ni Mhadhiri wa Uchumi SUZA Dk, Suleiman Simai Msaraka.
Meneja Msaidizi Uchumi Benki kuu ya Tanzania Tawi la Zanzibar Deagratias Philip Mache akijibu baadhi ya maswala yalioulizwa katika hafla ya kutoa Takwimu za Bei katika Ukumbi wa Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Mjini Unguja.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika hafla ya kutoa Takwimu za Bei katika Ukumbi wa Ofisi kuu ya Takwimu Mazizini Mjini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment