Advertisements

Tuesday, February 27, 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AAGIZA WAKURUGENZI KUPANDISHWA KIZIMBANI JIJINI MWANZA, NI KWA KUTOJISAJILI NA WCF

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde(kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, 9WCF), Bw. Anslem Peter, akitoa maagizo ya kufikishwa mahakamani mara moja mkurugenzi mtendaji wa Belmonte Hotel ya jijini Mwanza leo Februari 26, 2018 kwa kushindwa kutekeleza takwa la kisheria linalomtaka kujisajili na Mfuko huo. Naibu waziri ameonya waajiri wote nchini kuttekeleza wajibu wao kwani hakuna mahala pa kujificha na operesheni hiyo inaendelea mikoa mingine.
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, (wakwanza kushoto), Mkurugenzi wa Uenmdeshaji (Director of Operations), Anslem Peter, Afisa Kazi Mfawidi Mkoa wa Mwanza, Khadija Hersi, wakipitia nyaraka za Hoteli ya Belmonte ya jijini Mwanza kuona jinsi uongozi wa hoteli hiyo unavyotekeleza Sheria ya Fidia Kwa wafanyakazi, kwa kujisajili na Mfuko huo. Naibu Waziri alifanya ziara ya kushtuikiza kwenye kampuni kadhaa jijini Mwanza ambapo hoteli hiyo ilibainika kutojisajili na aliamuru Mkurugenzi wake kupelekewa mahakamani mara moja. Wakwanza kulia aliyesimama ni Mkuu wa KItengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge.
Naibu waziri akiongozana na Bw. Anslem Peter na afisa mwingine kutoka jijini Mwanza mara baada ya kukagua ofisi za huduma za vifuriushi na mizigo uwanja wa ndege wa Mwanza, Airco Holdings.
Mkurugenzi wa Belmonet Hotel ya jijini Mwanza, Bw.Philemon Tei
Naibu Waziri Mvunde, akizungumza na wafanyakazi wa Airco Holdings ya uwanja wa ndege wa Mwanza. Kushoto ni Bw. Anslem Peter
Naibu Waziri akiwa kwenye ofisi za Airco Holdings uwanja wa ndege wa jijini Mwanza
Naibu Waziri akitoa maelekezo kwa uongozi wa Belmonte Hotel
Maafisa wa WCF, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anslem Peter, (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, wakitoka kwenye kiwanda cha kuchakata samaki jijini humo baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza.
Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, ya jijini Mwanza Bw. Karan Bachu, akijieleza mbele ya Naibu Waziri Mvunde, (hayupo pichani)
Mhe. Mavunde, (kushoto), akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, ya jijini Mwanza Bw. Karan Bachu
Mhe. Mavunde, akizungumza na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya JASCO ya jijini Mwanza baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza leo Februari 26, 2018.
Mhe. Mavunde na maafisa wa WCF wakiwa ofisi za kampuni ya kuchataka samaki jijini Mwnaza
Mhe. Naibu Waziri akipitia nayaraka za kampuni ya kuchakata samaki ya jijini Mwnaza wakati wa ukaguzi wake.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anslem Peter akimuonyesha nyaraka za kampuni ya uchakataji samaki jijini Mwanza, ambayo imeanza kuwasilisha michango, lakini bado haijajisajili na Mfuko, ambapo aliagiza watekeeleze takwa hilo haraka.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Antony Mavunde, (pichani juu), ameagiza waajiri ambao hawajajisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kufanya hivyo, vinginevyo wafikishwe mahakamani mara moja.

Mhe. Mavunde ametoa agizo hilo Jumatatu Februari 26, 2018 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jijini Mwanza, kubaini waajiri ambao bado hawajatekeelza takwa la kisheria kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia Kwa Wafanyakazi, Sura 263 marejeo ya mwaka 2015, ambayo inamtaka kila mwajiri kutoka sekta ya umma na binafsi Tanzania bara awe amejisajili na kuwasilisha michango kwenye Mfuko huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter, jiji la Mwanza pekee lina waajiri 1228, lakini kati ya hao ni waajiri 482 tu ndio waliojisajili na Mfuko huku waajiri wengine 746 wakiwa bado hawajajisajili. Hali hiyo ndiyo iliyomfanya Mhe. Naibu Waziri kufanya ziara hiyo ya ghafla.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo wa kushtukiza, Mhe. Mavunde pia ameiagiza WCF kuwafikisha mahakamani mara moja, waajiri wa kampuni ya ujenzi ya JASCO, (Mkurugenzi Mtendaji Bw.Karan Bachu),

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Airco Holdings inayotoa huduma za kusogeza vifurushi na mizigo uwanja wa ndege wa Mwanza na hoteli ya Belmonte ya jijini humo ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli hiyo, Bw. Philemon Tei, amejikuta matatani.

"Naagiza waajiri hao kulipa michango yote ya nyuma (tangu tarehe 1 Julai 2015 tangu Mfuko ulipoanza kutekeelza majukumu yake au siku mwajiri aliyoanza kazi zake iwapo ni baada ya tarehe 1 Julai 2015).

Mhe. Mavunde ameagiza waajiri hao kufanya mawasiliano na watendaji wa Mfuko haraka iwezekanavyo ili kuweza kubaini kiwango cha riba kila mwajiri anachopaswa kulipa kutokana na kuchelewesha michango katika Mfuko. “Ni kosa la jinai kwa mwajiri kutotekelza takwa hilo la kisheria na kifungu cha 71(4) cha Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kimeweka wazi kuwa mwajiri wa aina hii, anaweza kutozwa faini isiyozidi shilingi milioni 50,000, kifungo kisichozidi miaka 5 jela au adhabu zote kwa pamoja, kwa hivyo nitoe wito kwa waajiri hao, hakuna sababu ya kushurutishwa kutekeleza sheria.
"Tutatekelza agizo la Mhe. Waziri kama alivyolitoa, na nitoe rai tu kwa waajiri kote nchini (Tanzania Bara), kutekeleza takwa hilo la kisheria, kwani hakuna kichaka cha kujificha tutawafikia." Alisisitiza Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anslem Peter katika taarifa yake kwa waandishi wa habari.

No comments: