Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika Mkutano huo Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wa nne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipokuwa ukipigwa katika ukumbi wa mkutano uliopo katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni wanne kutoka kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na Rais wa Sudani ya Kusini Salva Kiir wakati wa mkutano huo Maalumu wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unao endelea jijini Kampala.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda Yoweri Museveni akifungua Mkutano huo maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Kampala nchini Uganda.
Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya a Afrika Mashariki wakifatilia hotuba mbalimbali katika Mkutano huo maalum.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais wa Uganda, Yoweri Museveni katika picha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kulia, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, pamoja na Rais wa Sudan ya Kusini Salva Kiir mara baada ya Mkutano Maalum wa 19 wa Jumuiya hiyo uliofanyika Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan ya Kusini, Salva Kiir kabla ya kuanza kwa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa 19 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Kampala Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja katika eneo la Munyonyo Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Mkutano Maalum wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC unaojadili masuala mbalimbali ikiwemo Maendeleo ya Sekta ya Miundombinu na Afya. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment