Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Rajabu Saidi Yote (kulia), ambaye ni mkaazi wa Tandika Dar es Salaam, akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo.
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Tinna Sharon Masatu (kulia), ambaye ni mkaazi wa Mbezi Beach akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa katika promosheni hiyo.
Mshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Margareth Martin Hiza (kulia), ambaye ni mkaazi wa Ubungo, Dar es Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Jumla ya washindi 156 wamejinyakulia simu katika promosheni hiyo.
Add caMshindi wa Simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea Nyaka Nyaka Bonus, Daniel Joseph Swai (kulia), ambaye ni mkaazi wa Iala, Dar es Salaam akipokea zawadi yake kutoka kwa balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kushoto) pamoja na Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (katikati). Zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa katika promosheni hiyo.
Baadhi ya washindi zaidi ya 84 waliojinyakulia simu aina ya Tecno R6 katika promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus wakiwa katika picha ya pamoja na balozi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Tigo, Mina Ali (kati) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi. Jumla ya washindi 156 wa simu tayari wamepatikana katika promosheni hiyo ambapo zaidi ya simu 900 bado zinashindaniwa.
Zaidi ya simu 900 na bonasi za internet bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Februari 26, 2018 – ‘Kwa sasa mama yangu anatumia simu ya kawaida ambayo haituwezeshi kuwasiliana kikamilifu kwa njia ya mtandao. Kwa mfano siwezi kumtumia picha za wajukuu wake. Ndio maana nitampa zawadi ya simu hii mpya niliyoshinda kutoka Tigo leo ili iturahisishie mawasiliano yetu na kumfanya awe sehemu ya ulimwengu wa kisasa wa mawasiliano.’ Haya ni maneno ya Margareth Martin Hiza, mfanyabiashara na mkaazi wa Ubungo jijini Dar es Salaam ambaye aliibuka moja wa washindi wa simu mpya za kisasa senye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 4G katika promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa na Tigo Tanzania.
Wateja wa Tigo Tanzania wanazidi kupata faida lukuki ikiwemo bonasi za hadi GB 1 bure kwa matumizi yao ya intaneti pamoja na fursa ya kushinda mojawapo ya simu janja 900 ambazo bado zinashindaniwa katika Nyaka Nyaka Bonus, promosheni murwa inayowazawadia wateja wa Tigo wanaounua vifushi vya kuanzia TZS 1,000 vya intaneti kupitia menu iliyoboreshwaya *147*00#.
Akikabidhi zawadi kwa washindi wa wiki hii, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema kuwa bado kuna zaidi ya simu 900 aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G ambazo zinashindaniwa na wateja watakaonunua vifurushi vya intaneti vya kuanzia TSH 1,000 kupiita menu *147*00#.
‘Washindi wetu wote 156 tuliowapata kufikia sasa wanatoka sehemu mbali mbali za nchi, kwa hiyo ninawashauri wateja wetu kote nchini washiriki ili wajishindie bonasi za data bure pampoja na mojawapo ya simu zaidi ya 900 za Smartphones ambazo bado zinashindaniwa,’ Woinde alisema.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
No comments:
Post a Comment