ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, February 25, 2018

USAJILI KILI MARATHON WAPATA MUAMKO MKUBWA MLIMANI CITY


Mbio za mwaka huu, ambazo zinaandaliwa na Wild Frontiers na Dep Blue Media na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions, zitafanyika katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (MoCU) Machi 4 kuanzia saa 12 asubuhi.
Wakazi wa Dar es Salaam wakijiandikisha kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zitakazofanyika Mjini Moshi Machi 4, mwaka huu. Zoezi hilo lilifanyika katika viwanja vya Mlimani City.


Usajili wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zinazotarajiwa kufanyika jumapili ijayo mjini Moshi umekuwa mkubwa huku wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani wakimiminika kukamilisha zoezi hilo na kupokea namba zao za ushiriki.

Zoezi hilo limefanyika kwa ukamilifu Jumamosi na Jumapili katika Viwanja vya Mlimani City ambao walidhamini eneo hilo la kujisajili kama njia ya kuunga mkono juhudi za kukuza na kuendeleza michezo hususan riadha.

“Tumeridhishwa sana na muitikio wa watanzania na kwa kweli mwaka huu muamko ni mkubwa zaidi kwani mbio hizi zimezidi kuwa maarufu na kubwa mwaka hadi mwaka,” allisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa mbio hizi.

Alisema wana uhakika washiriki watazidi 10,000, idadi ambayo ilifikiwa mwaka jana. “Mwaka huu sisi kama Kilimanjaro Premium Lager tunawakumbusha wateja wetu kuwa twende Moshi kushiriki, tufurahie bia yetu namab moja baada ya kukimbia lakini pia tukumbuke kutoendesha vyombo vya moto huku tukiwa tumetumia kilevi,” alisema Meneja huyo.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema wao kama wadhamini wa mbio za kilometa 21wameona muamko mkubwa na wanatarajia washiriki wengi zaidi katika mbio hizo za half marathon.

“Muamko ni mkubwa sana na tunashukuru watanzania kwa kendelea kutumia Tigopesa kujisajili ila tunasisitiza walipie ili kuthibitisha ushiriki wao kwa kukabidhiwa namba za ushiriki kuna ambao wanajisajili lakini hawalipii ada ya ushiriki,” alisema.

Naye Meneja Masoko wa kinywaji cha Grand Malt, Warda Kimaro, ambaye kinywaji chake kinadhamini mbio za kilometa tano maarufu kama Fun Run, alisema, “Kwa kweli muamko wa mwaka huu unatia moyo na inaonesha jinsi gani watu watafurika Moshi kushiriki mbio hizi Machi 4mwaka huu. Mbio za Kilometa 5 ni kwa wshiriki wa rika zote hivi tunawaomba waendelee kujisajili kwa wingi na tukutane Moshi Jumapili ijayo,” alisema.

Baada ya Dar es Salaam, usajili Arusha utafanyika Februari 27 na 28 katika hoteli ya Kibo Palace kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi na moja na Moshi ni Machi 1 kuanzia saa sita mchana hadi saa moja usiku, Machi 2 kuanzia saa nne asubuhi hadi saa moja jioni na Machi 3 kuanzia saa tatu hadi saa sita mchana.

Wadhamini wengine ni pamoja na First National Bank, Kilimanjaro Water, Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Simba Cement, KNAUF Gypsum na AAR as ambao ni wabia katika masuala ya tibabu.

No comments: