Advertisements

Tuesday, February 13, 2018

Wakazi Mwananyamala wavutiwa na huduma za 'One Stop Centre' za CRC

Mwanasheria wa Kituo cha Usuluhishi–CRC, Suzan Charles (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jana jijini Dar es Salaam.
Afisa wa Polisi na Mratibu wa Kituo cha One Stop Center (OSC) Amana, Bi. Christina Onyango (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma leo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wahudumu wa afya kwenye kituo hicho akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika kupata huduma.
Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.
Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.

Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wananchi wanaoishi Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam wamevutiwa na huza huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na msaada wa ushauri kisheria zilizotolewa jana na Kituo cha Usuluhishi – CRC.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi waliopata huduma hizo kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mwananyamala 'A' walisema wamefurahishwa na kitendo cha CRC kusogeza huduma hizo eneo lao jambo ambalo limewavutia wakazi wengi.

"...Binafsi nimevutiwa na kitendo cha huduma kama hii kutolewa eneo letu, mimi nilikuwa na kesi kuna mtu anataka kunidhulumu kiwanja kesi yangu inaendelea lakini baada ya kuona kuna huduma hizi nimekuja kupata msaada wa kisheria na nimeshauriwa cha kufanya...,"alisema Bi. Nzela Khamis akizungumza mara baada ya kuhudumiwa.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Usuluhishi – CRC, Bi. Violeth Chonya akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema Mwananyamala kumekuwa na  muitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Alisema jumla ya kesi 31 wamezisikiliza na kufikia hatua mbalimbali huku kesi mbili za matuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande zote mbili na wazazi kufikia muafaka juu ya mvutano wao.

Bi. Chonya alisema kwa muitikio wa wananchi wa leo umeonesha kuna uhitaji mkubwa wa huduma hizo hivyo kuwashauri wananchi wa Mwananyamala kujitokeza tena kesho ambapo huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na ushauri wa kisheria utatolewa.

"...Kimsingi bado uhitaji ni mkubwa hivyo tunawashauri kesho wananchi wanaohitaji huduma hizi wajitokeze tena kesho tunaendelea kutoa huduma zetu, na baadhi ambao watashindwa kuja kesho wanaweza kuja ofisi za TAMWA Sinza Mori kwenye ofisi zetu (CRC) watahudumiwa pia," alisema Bi. Chonya.

No comments: