ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 26, 2018

WATAALAM WA AFYA MOJA WAJIPANGA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI NCHINI

 Mtaalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Jacob Lusekelo akiwasilisha mada juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi , wakati wa mkutano wa wataalam wa afya moja mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu (wa kwanza) akifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usaama wa vimelea hatarishi mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
 Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakifuatilia mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Wataalamu wa Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.


Na. Mwandishi Maalum

Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wamejipanga kudhibiti vimelea hatarishi kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo .

Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa kuvichukua kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Akiongea wakati wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiri Taratibu alibainisha kuwa serikali kupitia Dawati la uraribu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imeamua kuandaa mpango wa kudhibiti vimelea hivyo ambavyo husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii na pia kamati maalum ya wataalam hao imeundwa iili kuufatilia na kusimamia mpango huo.

“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Maafa ndiyo yenye dhamana ya kuratibu maafa kama ya magonjwa ya mlipuko kama kimeta, Hivyo jitihada za serikali za kuwakutanisha wataalam hawa ili ni kuweza kuijenga jamii salama ambayo haiathiriki na magonjwa yanayotoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia mpango huu.” Alisema Taratibu.

Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph Masambu walibainisha kuwa kuandaliwa kwa mpango wa kuzishirikisha sekta zote za afya kutaimarisha afya za binadamu kwakuzingatia kuwa upo mwingiliano mkubwa kati ya binadam na. wanyama.

Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu ,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Shirika DTRA wameandaa mkutano wawadau hao.

No comments: