Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Seleman Jafo akizungumza na wananchi wa kijiji cha kimara misale iliyopo kata ya Mafizi Wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbai mbai ya maendeleo na kuweza kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili wananchi ii kuweza kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wakiwa katika mkutano wa adhara kumsikiliza Waziri jafo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kujionea miradi mbai mbali ya kimaendeleo inayotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na nguvu za wananchi wenyewe.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amesema hawezi kuwavumilia hata kidogo baadhi ya wawekezaji ambao wamekuwa na tabia ya kufanya udang’anyifu kwa wananchi kutokana na kuchukua maeneo makubwa ya ardhi pasipo kuyaendeleza mpaka yanapelekea kuwa mashamba pori hivyo ameagiza yarudishwe katika mikono ya serikali za vijiji ili wananchi wenyewe waweze kuyaendeleza katika shughuli nyingine za kimaendeleo.
Jafo ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa wananchi wa kijiji cha Kimara Misale kilichopo kata ya Mafizi katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe ambapo amekwenda kwa ajili ya kuweza kujionea na kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuweza kusikiliza changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa jimbo lake.
Amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la mashamba pori katika baadhi ya maeneo ambayo kwa kipindi cha muda mrefu yametelekezwa hivyo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa lengo la kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kurudishiwa maeneo yao ambayo yamechukuliwa na watu wachache ambao wameshindwa kabisa kuyaendeleza kama inavyostahili.
Aidha Waziri Jafo katika hatua nyingine ametoa muda wa siku 30 kwa watendaji wa idara ya ardhi ya halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha wanamaliza mgogoro wa mipaka ya ardhi uliopo baina ya wananchi wa kijiji cha Kimara misale kata ya mafizi na baadhi ya vijiji vingine ambavyo vipo katika halmashauri ya Kibaha vijijini.
Awali baadhi ya wananchi hao akiwemo Issa Zoka na Salumu Hombo wakitoa malalamiko yao kwa niaba ya wenzao kwa Waziri katika mkutano wa adhara wamesema kumekuwepo na migogoro kila kukicha ya kugombania mipaka ambayo inachangia wakati mwingine kutoelewana kwa watendaji na viongozi katika suala la ukusanyaji wa mapato na mambo mengine ya kufanya maendeleo.
KUWEPO kwa ongezeko la mashamaba pori katika baadhi ya maeneo hapa nchini hususan katika Wilaya ya Kisarawe iliyopo Mkoa wa Pwani ni kutokana na baadhi ya wawekezaji kununua ardhi kwa makubaliano ya kuwekeza katika ujenzi wa huduma mbali mbai za kijamii ikiwemo shule, zahanati, masoko lakini mwisho wa siku wanayatelekeza na wengine kuyatumia kuchukulia mikopo benki.
No comments:
Post a Comment