ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 26, 2018

Atiwa Mbaroni Kwa Kuwabaka wanawake na Kuwapiga Picha za Uchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemkamata mkazi wa mjini humo, Mabula Mabula maarufi Six kwa tuhuma za uporaji wa simu kwa kutumia pikipiki, kubaka na kuwapiga picha za utupu wanawake kisha kuzisambaza mitandaoni.

Akizungumza leo Jumatatu Machi 26, 2018, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa baada ya makachero, kikosi cha kupambana na uhalifu  mitandaoni pamoja na kikosi cha kupambana na ujambazi, kumfuatilia kwa ukaribu.

Akihojiwa mara baada ya kukamatwa, Mabula ameeleza mbinu anazotumia ikiwa ni pamoja na kujifanya askari polisi, kuwakamata wanawake nyakati za usiku, kuwasingizia makosa mbalimbali na kuwapeleka maeneo yenye giza na kuwabaka.

Mtuhumiwa huyo ameyataja maeneo anayofanyia matendo hayo kuwa ni Msamvu Relini na kwamba amekuwa akitumia mapanga kuwatisha wanawake hao na kuwapiga picha za utupu na baadaye kutishia picha hizo kuzituma kwenye mitandao ya kijamii.


“Hizo picha huwa nawapiga kwa kutumia simu zao na anayekataa kunipa hela huwa naondoka na simu yake na kisha natuma hizo picha kwenye mitandao iliyopo kwenye simu hizo, baada ya hapo simu naiuza napata hela,” amesema mtuhumiwa huyo.

Katika  mahojiano na polisi, mtuhumiwa huyo amemtaja mwezake mmoja Ramadhani Salumu maarufu Miondoko mkazi wa Manispaa ya Morogoro kuwa ndio mnunuzi wa simu hizo za wizi.

Katika msako huo polisi wamefanikiwa kumkamata Salumu na kwamba wote watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments: