Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (kushoto), akiwa ameambatana na mwenyeji wake mmiliki wa Yatch Club Bw. Brian Fernandes (kulia), baada ya kuwasili ofisi za Yatch Club kwa ajili ya uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CF) Billy Mwakatage (wa pili kushoto), akiwa na wakufunzi kutoka nchini Ujerumani na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. Alipotembelea eneo hilo mapema leo asubuhi.
Mkufunzi kutoka nchini Ujerumani Bw. Dan Jungingfer (kulia), akitoa maelekezo ya mbinu za uzamiaji majini kwenye kina kirefu kwa Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Sajini Gift Longwe na Konstebo Baltazari Swai. Wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uzamiaji majini kina kirefu daraja la pili kwa Askari wa Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Zimamoto Na Uokoaji)
Mafunzo haya yanayoendeshwa hapa nchini na Wakufunzi kutoka Ujerumani yana lengo la kuwaongezea Maafisa na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji weledi katika kukabiliana na majanga ya mafuriko na kuzama kwa watu majini haswa kwenye kina kirefu.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
No comments:
Post a Comment