Advertisements

Friday, March 2, 2018

Upelelezi bado kesi ya kina Rugemalira

Upande wa mashtaka katika kesi inayowakabili Habinder Sethi na James Rugemalira umedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola 22.198 milioni za Marekani (Sh309.5 bilioni) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwendesha mashtaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai amedai hayo mahakamani leo Machi 2,2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati shauri lilipotajwa.
"Upelelezi wa kesi hii bado haujakamilika, hivyo tunaomba Mahakama ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa," amesema Swai.
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 16, 2018 itakapotajwa. Washtakiwa wamepelekwa rumande.

No comments: