Waziri mwenye dhamana na wizara ya nishati ndugu Dr. Medard Kalemani (MB), ametembelea kiwanda kipya cha kutengeneza mita za umeme kiitwacho Baobab Energy Sytems Tanzania, kilichopo eneo la mbezi juu Dar es salaam, kinachomilikiwa na watanzania. Akizungumza katika uzinduzi huo, mheshimiwa waziri amesifu uwekezaji uliofanywa na watanzania hawa, na kueleza wazi kwamba hiki ni kiwanda cha kwanza chenye teknolojia chanya inayolenga kusaidia tanzania kuokoa gharama za manunuzi ya mita na vifaa vya umeme kutoka nje ya nchi.
Katika maeleze yake, mheshimiwa Dr.Medard Kalemani(MB). Waziri ameipa Tanesco miezi 3 kuhakikisha wanasitisha ununuzi wa mita za umeme kutoka nje ya nchi kwani tayari viwanda vya ndani kikiwamo Baobab vimeonesha kuwa na uwezo wa kuzalisha kukidhi mahitaji ya nchi. “kwa sasa kiwanda kinauwezo wa kuzalisha mita za umeme elfu thelathini na nane(38000) kwa mwezi, wakati mahitaji ya tanesco ni mita elfu ishirini kwa mwezi (20000), hivyo naipa tanesco miezi mitatu waangalie kazi inayofanywa na wataalamu hawa na waanze kununua mita hizo kutoka kwa wazalishaji hawa wa ndani”. Kwa sasa nchini tanzania kuna viwanda viwili vya uzalishaji wa mita za umeme, Baoba ikiwa ni kiwanda kimoja wapo
Pia mheshimiwa waziri ameiagiza tanesco kushirikiana na wazalishaji hawa wa mita za umeme ili kupunguza ulazima wa kupeleka mita na vifaa kama hivi nje ya nchi kwaajili ya matengenezo pindi vinapo haribika.
Mkurugezi mkuu wa Baobab Energy Systems Tanzania ndugu, Eng.Hashim Ibrahim amesema kwamba wamewekeza katika uzalishaji huu wa mita za umeme, kwani wameona changamoto kubwa serikali iyopata kuagiza mita kutoka nchi nyingine, jambo ambalo linapelekea uhaba wa
Mita hizi zinazozalishwa nchini zina ubora wa kipekee unaoweza kutambua mwizi wa umeme, upotevu wa umeme na pia zinapatkana kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na gharama ambazo kwa sasa zinatumika kununua mita hizi.
Mkurugenzi mkuu wa Baobab Energy Systems Tanzania ndugu Eng. Hashim ibrahim ameahidi kwamba kiwanda hichi kimelenga kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania hasa wanaohitimu vyo mbalimbali hapa nchini vikiwamo veta. Pia ameeleza kwamba malengo mapana ya uanzishaji wa kiwanda hichi pia ni kusaidia jitihada za mheshimiwa rais wa awamu ya tano Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwenye sera yake ya uwekezaji wa viwanda.
No comments:
Post a Comment