ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 3, 2018

Halima Mdee Naye Kapata Dhamana kwa Bondi ya Milioni 20

Mbunge wa Kawe Halima Mdee leo April 3, 2018 alifikiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa na akina Freeman Mbowe
Mdee  yeye alisomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Mahakama imempa  dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20 na kuripoti mara moja kila wiki.


Mahakama  imesema haiwezi kumnyima mshtakiwa dhamana kwa sababu aliruka dhamana ya polisi maana  polisi ni taasisi nyingine na mahakama ni taasisi nyingine, hivyo ikampatia dhamana mshtakiwa kwa masharti tajwa hapo juu.

No comments: