|
|
Ubalozi wa Marekani
Dar es Salaam
TANZANIA
|
4 April 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Marekani na Tanzania Zashirikiana
kukabiliana na Ujangili na Usafirishaji Haramu wa Wanyamapori
Dar es Salaam: Tarehe 4 Aprili
2018, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson alikabidhi rasmi kwa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) magari matatu aina ya Toyota Land Cruiser kama sehemu ya programu ya
Serikali ya Marekani ya Mafunzo na Kujenga Uwezo wa Kukabiliana na Ujangili na
Biashara Haramu ya Usafirishaji Wanyamapori.
Kukabidhiwa kwa magari haya TAWA
kunaongeza uwezo wa askari wake wa wanyamapori kufanya doria za kuzuia ujangili
katika mapori ya akiba ya Rungwa/Kizigo/Muhesi na kuthibitisha ushirikiano
endelevu na imara kati ya Marekani na Tanzania. Akizungumza katika hafla ya
makabidhiano hayo, Kaimu Balozi Patterson alisema kuwa, “kwa ushirikiano wa
dhati kati ya serikali, raia wake, wabia wa maendeleo, asasi za kiraia na sekta
binafsi, tunaweza kulikabili na kulitokomeza janga hili la ujangili na
usafirishaji haramu wa wanyamapori.”
Serikali ya Marekani ni mbia
mwenye fahari katika jitihada za Tanzania za kukabiliana na ujangili na
usafirishaji haramu wa wanyamapori, ambapo imekuwa ikitoa mafunzo, vifaa na kufadhili
shughuli za kujenga uwezo (capacity building) ili kuongeza uwezo wa askari
wanyamapori kudhibiti ujangili katika mapori ya akiba ya Rungwa,Kizigo naMuhesi. Miradi inayofadhiliwa hivi sasa na serikali
ya Marekani ni pamoja na ule wa kuweka mfumo wa Mawasiliano ya simu, ukarabati
wa vituo viwili vya askari wanyamapori na kuweka daraja maalumu la kamba
kuwezesha kuvuka mto katika kipindi chote cha mwaka kuelekea mashariki mwa
hifadhi. “Mafanikio yaliyopatikana hivi
karibuni yanatupa matumaini,” alisema Kaimu Balozi Patterson, “hata hivyo bado
vita dhidi ya ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori haijamalizika.
Serikali ya Marekani ina fahari kusimama pamoja nanyi katika vita hii.”
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya
Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au
kwa barua pepe: DPO@state.gov.
Jitihada za Serikali
ya Marekani za Kukabiliana na Ujangili na Biashara Haramu ya Usafirishaji
Haramu wa Wanyamapori:
Mwezi
Oktoba 2016, Rais Mstaafu Barack Obama alisaini Mswada wa Sheria ya Kutokomeza,
na Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Wanyamapori kuwa sheria kamili. Sheria hii ilipitishwa
bila kupingwa na wajumbe kutoka vyama vyote kwa kuwa inaielekeza Serikali ya
Marekani kuendelea kutoa misaada ya kiusalama kusaidia jitihada za kukabiliana
na usafirishaji haramu na kuhakikisha pana uratibu mzuri kati ya taasisi
mbalimbali za Serikali ya Marekani na balozi za Marekani katika nchi mbalimbali
katika kushughulikia suala hili.
Kupitia ushirikiano wake na
TAWA, Ubalozi wa Marekani unalenga kusaidia uhifadhi wa wanyamapori na maeneo
yao kupitia shughuli mbalimbali zilizoratibiwa. Kwa miaka mitatu sasa,
ushirikiano huu rasmi umejielekeza katika kushirikiana na askari wanyamapori
katika kupanga na kutekeleza doria mahsusi, zinazowapo walinzi wa Kitanzania wa
wanyamapori taarifa zinazowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu. Kazi
hii inahitaji vifaa na serikali ya Marekani inachangia kwa kuwapa askari
wanyamapori ramani, Mifumo ya utambuzi wa maeneo ya GPS, matrekta na matela
yake pamoja na kukarabati vituo vya askari hao (ranger posts).
No comments:
Post a Comment