Mahakama ya Wilaya ya Dodoma leo Aprili 5, 2018 imepokea taarifa ya vipimo vya kitabibu vya Tito Machibya (Nabii Tito) ili kujua kama ana matatizo ya akili au la.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha leo Alhamisi Aprili 5, 2018 amesema amepokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito kutoka Isanga hivyo ataipitia ili aje atoe maamuzi siku ya April 13 mwaka huu.
“Niseme tu kuwa nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu mtuhumiwa leo asubuhi hivyo nitaipitia ili April 13, 2018 siku ya ijumaa niweze kuitolea maamuzi,” amesema Karayemaha.
Nabii Tito ambaye hakuweza kuhudhuria kesi yake mara mbili mfululizo leo amefika mahakamani baada ya hakimu Karayemaha kutoa maagizo ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani au aletewe taarifa rasmi ya kwa nini hafikishwi mahakamani kusikiliza kesi yake.
Nabii Tito amerudishwa rumande hadi Aprili 13 kesi yake itakapotolewa uamuzi.

No comments:
Post a Comment